Blogger Widgets

July 24, 2012

“NIMEFUNGA MWEZI MTUKUFU LAKINI NAENDELEA KUFANYA MUZIKI KAMA KAWA” – ISHA MASHAUZI…!!



MSANII anayefanya vizuri kwenye muziki wa taarabu nchini Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, amesema kuwa amefunga kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani lakini haimanishi kwamba amefunga na shunguli zake za muziki kwani hizo ndizo zinazompa kula mjini na kuendesha familia.

Akiongea na DarTalk msanii huyo alisema kuwa muziki kwake ni kazi hivyo endapo akisimama mwezi mzima anaweza kufa njaa, hivyo anaendelea na muziki na hata akipata show kipindi hiki anafanya kwa lengo la kutoa burudani kwa mashabiki wake.


Alidai kuwa kikubwa atatumia kipindi cha mwezi mtukufu kuangalia safu yake ya uimbaji ili kuweza kuiweka katika kiwango kizuri zaidi.


“Mwezi mtukufu haimanishi kwamba hata muziki pia watu wanafunga hapana kikubwa ni kumuomba mungu na kutubu makosa yetu kwani, hiki ni kipindi kizuri cha kutafakali kila hatua ambayo tumepitia,”

No comments:

Post a Comment