Blogger Widgets

July 29, 2012

ONLY AND ONLY IN THIS BLOG:Kisa cha Mfanyakazi Mrembo alibadilika kuwa kahaba Wa kutupa kuwaambukiza watu HIV.Unajua nini chanzo?


SIMULIZI YA KAHABA


Nilikua mwajiriwa katika
kampuni moja maarufu jijini
dare s salaam , katika
kuajiriwa kwangu huko
nikawa msaidizi maalumu wa
bosi wa kampuni ile , basi siku moja moja nilikuwa
naenda kujirusha na bosi
wangu .

Ukizingatia kwamba sikuwa
na mume wala mchumba na
kwa kweli huyu bosi ndio
alikuwa mtu wa kwanza
kufanya nae tendo la ndoa ,
hivyo nilifurahia mhemko wake na jinsi alivyokuwa
ananipenda na kunijali kila
kitu nilipata na zaidi .

Alifanya yote haya bila
kunificha kwamba ana mke
na watoto nyumbani kwake
kwahiyo wakati mwingine
chochote kinaweza kutokea
nijiandae kwa shuguli hiyo pevu kama mke wake
akishitukia dili hilo .


Tulikuwa na uhusiano na huyu
bosi kwa miezi 4 hivi mpaka
siku moja katika tembea
tembea mitaani nikakutana
na kijana mmoja mtanashati
akanieleza kwamba ananipenda na kunizimia
sana yaani ameshanifia


Huyu kijana alihangaika kwa
mwezi mzima mpaka siku
nikaja kumkubalia akawa
ndio mpenzii wangu halali
sasa , nilimwamini sana nay
eye aliniamini sana , miezi 3 tokea kujuana na huyu kijana
aliniambia kuhusu kufanya
nae tendo la ndoa .

Nilifikiria sana wakati
mwingine nilitaka kulia jinsi
alivyokuwa ananishika na
kuniomba tendo la ndoa
akiwa chumbani kwangu ,
alijaribu kunishika sehemu kadhaa akanivua nguo nami
nilimtolea nje nilimkatalia .

Basi siku moja nikamwomba
tukaangalie afya zetu , kijana
wa watu alikasirika sana wiki
nzima hakufika nyumbani
kwangu wala kunipigia simu ,
kumbe alitaka tufanye tendo la ndoa bila kinga ? sasa
ningejuaje kuhusu afya yake ?
au ananiamini nini mimi ?

Maisha yaliendelea na mambo
mengine yaliendelea tu wiki
ya 3 alinipigia simu
akaniomba msamaha
turudiane na alikubali
kwenda na mimi kupata vipimo vya afya zetu kujua
kwanza kabla hatujaanza
mambo mengine yoyote yale .


Basi ndio hivyo majibu
yaliyoka mazuri , ndio
mapenzi yetu alikuwa zaidi
na penzi nilimpa bila hiyana
wala aibu yoyote , yeye
mwenyewe alifurahia mambo yangu na kwanza alikuwa
anatoroka nyumbani kwao
kuja kulala kwangu wakati
mwingine mwezi mzima .

Tuliendelea kwa miezi kadha
na huyu kijana huku na mimi
nikiwa na bosi wangu kule
kazini , basi bwana siku
moja , sisi officini tulitakiwa
kwenda kutoa damu hospitali ya muhimbili katika
maadhimisho ya siku ya afya
duniani .

Watu walipimwa afya zao na
mimi nilipimwa , majibu
yangu yalikuwa ya
kutatanisha sikuamini macho
yangu wala masikio yangu ,
nilienda hospitali ingine napo majibu yalikuwa yale yale
kwamba nimeadhirika na
UKIMWI .


Haya majibu yalimfikia
mpaka bosi wangu nae
akatambua hilo akasikitika
sana nay eye alivyoenda
kupimwa akakutwa
hajaadhirika , basi nikajua moja kwa moja ukimwi
nimepata kutoka kwa yule
kijana wa mitaani na sio mtu
mwingine .


Nikamwomba huyu kijana
tukaangalie afya zetu kwa
mara ingine tena hospitali ,
tukaenda kule kupima afya
zetu , yeye ndio alikuwa wa
kwanza kupokea majibu yake , alikutwa ameadhirika
akupata mshituko wa ghafla
yaani haamini . Mshituko huo ulimpelekea
aanguke chini na kuzimia
watu walienda kumbeba na
kumpeleka hospitali
kupatiwa huduma ya kwanza
basi hapo ndio magonjwa mengine yalianza kujitokeza
na kujulikana sana .


Kumbe huyu kijana alikuwa
na urafiki wa kimapenzi na
shugamami mmoja mtaa wa
pili huyu shuga mami mume
wake alifariki dunia miaka 5
iliyopita kwa UKIMWI watu wanaema TB sijui , ndio huyu
kijana kuona zile pesa za
shuga mamy akaenda
kwake . Kijana aliumwa kwa miezi 3
hivi kisha akafariki dunia
akaniacha duniani
mwenyewe , kule kazini
nilifukuzwa kaza na bosi
wangu kisa nilitaka kumwambukiza ugonjwa wa
ukimwi , lakini siku moja
alinipigia simu kunieleza
kwamba mke wake
ameadhirika na UKIMWI pia
lakini yeye anasema hajaadhirika .


Hapo ndio nilishangaa sana ,
kwanini mke wa aadhirike
yeye asiadhirike au mke
wake nae alikuwa anatoka
nje ya ndoa bila mume wake
kujua ? basi hiyo ni siri yao nyumbani kwao mimi
hayanihusu . Lakini ndio hivyo nilikuwa
nimeshaadhirika na UKIMWI
kazi nimeshafukuzwa sina
cha kufanya wala kutafakari
nilifikiria zaidi kuhusu
ugonjwa wangu wa UKIMWI na jinsi nitakavyoweza kuishi
maisha marefu kwa
matumaini .


KAHABA

Baada ya kuona maisha
magumu na sina lolote la
kufanya mimi kama
mwanamke mrembo na
mwenye mvuto niliamua
kutafuta njia rahisi zaidi ya kujipatia kipitano nilifikiria
njia nyingi sana ambazo
zingeweza kunipatia angalau
mlo na mavazi katika siku
zangu za maisha zilizobakia
baada ya kugundulika nina virusi vya ukimwi Nikaanza kutafuta sehemu
ambazo naweza kuuza mwili
wangu kwa pesa za chapchap
niweze kuendeleza maisha
yangu ya kila siku , nilikuwa
na ramani yangu kwanza pale OHIO , JOLLY , MACHENI , BILLS
NA LATAVERNA hizo ni
sehemu 5 kuu za starehe
jijini dare s salaam kwahiyo
huko naweza kufanya kazi za
kujiuza kwa wiki nzima kila siku bila kuchoka .


Ohio ilikuwa nzuri ila tatizo
lake ni kwamba kila
anayepita pale anakujua
halafu unatakiwa uonyeshe
maungo yako hazarani mimi
sikuzoea tabia hizo na sikuwa na mhemko huo
kwahiyo nilivaa miwani
yangu na kuacha mapaja nje
tu waangalie wenyewe kama
wanapenda watakuja .
Kule macheni tatizo lake ni mashoga wengi sana , yaani
mwanaume anaweza akaja
kutafuta Malaya
akakuchanganya wewe ni
shoga , wale mashoga
wanaojiuza hawana tofauti na sisi wanawake tunaojiuza
wakati Fulani ulitokea
ugomvi mkubwa watu
waliamulia tulimgombea
mwanaume .


Billa nako kuzuri ila vijana
wengi sana halafu hawana
pesa , na vitoto vidogo vingi ,
nilikuwa naogopa matatizo
na vijana wa kule sikupenda
kufanya mchezo na watoto wadogo waliokuwa
wananitaka hata kwa dau
gani nilingoja wanaume
wenye pesa zao tu sio zaidi . Basi nilianza safari za
kuelekea jolly club kwa ajili
ya kujiuza mwili wangu
nipate angalau chochote cha
kula na kufanya katika
maisha yangu , pale jolly club nilikutana na dada mmoja
anaitwa Aisha , huyu dada
nae ni kahaba mzoefu
akaanza kunionyesha mambo
kadhaa wa kadha kuhusu
biashara ya ukahaba na kadhalika .
Hapa ndio nilijufunza
kwamba sio makahaba wote
ni masikini au hawajiwezi
kuna wengine wanajiweza na
wanazo fedha ila wanapenda kufanya ukahaba yaani
wamechoka na dunia
wengine walikuwa na
wanaume wao wakaachika
wakaamua kuja huku
kwenda na mwanaume wowote yule anayekuja .



Wengine wana matatizo
katika ndoa zao kupigwa na
kadhalika wanaamua kuja
huku kujiuza au kukaa huku
ili kuepuka matatizo katika
ndoa zao au mahusiano yao , wengine ndio kama hivyo
waume zao hawana nguvu za
kutosha kufanya nao tendo la
ndoa wanaamua kuwa
makahaba kila mtu na lake
na mambo yake pia . Wengine wanafanya huu
ukabaha kwa ajili ya
kupeleleza yaani ni
wapelelezi wa polisi au watu
Fulani katika serikali wako
katika mitaa hii kuzuga tu , ili wafanikishe kazi zao za
uchunguzi kama polisi wa
usalama sehemu walizoko .


Mwisho wa yote siku hizi
kuna vita kubwa katika
biashara hii ya ukabaha mjini
dare s salaam , mfano kule
jolly kuna wazungu na
wahindi wanakuja kufanya biashara ya ukahaba kwahiyo
wewe mwamfrika unakazi
ngumu kuwapita wale
wazungu na wahindi au
wachina .

Siku hizi wanaume wengi
wanapenda kitu kinaitwa
JICHO yaani kufanya mapenzi
kinyume na maumbile , hii
nayo ni soko kuu , mfano
mwingine anaweza kuja kwako anataka jicho na
wewe hutoi jicho maana yake
unakosa soko suluhicho ni
kujitoa mhanga na kufanya
mapenzi kwa kuwa mteja ni
mfalme . Mbaya zaidi kuna wanaume
wengine wanakuja
wanaweza kukuchukua
uende nao kufanya ngono
kumbe wanakupiga filamu za
ngono wakati unafanya kitendo hicho haswa
wazungu wengine wanakupa
ufanye mapenzi na mbwa
wao au wanyama wao
wengine mambo yanaenda
hivyo .


Biashata hii ya ukahaba
ilinichanganyia sana kwa
miaka 2 niliyoifanya na kwa
kweli hakuna aliyenijua kama
nimeadhirika na ugonjwa wa
ukimwi nilikuwa najitunza na kutuza siri zangu hizi kuu na
sikupenda kuzoeana na watu
sana hadi waniulize hivyo Siwezi kuhesabu ni watu
wangapi nimefanya nao
ngono lakini ni zaidi ya 300
siku zingine nafanya kazi na
watu zaidi ya 3 kwa siku
moja kwahiyo mambo yanaendelea halafu wengi
hawakupenda kutumia
mipira ya kiume yaani kondo
walipenda kuja hivi hivi tu
bila kinga chochote kile


Na mimi nilikuwa
nimeshaadhirika nilichokuwa
natafuta ni fedha za
kuendeleza maisha yangu
kwahiyo hata kama nikifanya
ngono zembe bila kinga mimi hainiumi sana kwa kuwwa
nilishajua hali yangu
sikuweza kuitengua siku wa
chochote cha kufanya zaidi ya
hichi . Hii ilikuwa ni kulipiza kisasi
kwa maasi ambayo yule
kijana alinifanyia
kuniambukiza UKIMWI kwa
makusudi huku akijua kabisa
ameadhirika siku nyingi ,kwakuwa yeye
ameamua kuniuwa mimi basi
na mimi nauwa wengi zaidi
na sijali kuhusu dhambi hizi
nilizozifanya na sijutii
kabisa .


MAISHA YA MTAANI

Huku mitaani waliniita
majina kama JLo wakati
mwingine salma hayek yaani
wale waigizaji maarufu
duniani kwa urembo nilio nao
na mvuto wake , hakuna hata mmoja aliyekuwa na mawazo
kama nimeadhirika au la kwa
maana yule kijana niliyekuwa
nae kama mpenzi alikufa kifo
cha ghafla watu walisema
amekufa kwa pressure . Mitaani napo nilikamua
kinoma , waume za watu
walikuja mpaka mlangoni
kwangu na magari yao ,
wananipakia na kunipeleka
katika kumbi za starehe na sehemu nyingine nyingi sana
wengine walinihonga mali na
mambo kibao kisa
wamenipenda wanataka
ngono


Na kwa uhakika hawa
wanaume niliwapanga sawia
kabisa na hakuna aliyeweza
kutambua mimi nina
wanaume wangapi na
wanaishi wapi wengi walijua ni washirika wangu katika
kazi zangu na mambo yangu
mengine kwanza sikupenda
kuongea na mwanaume
wowote chumbani kwangu
wote nilikuwa nawaambia tukutane mbali kidogo na
nyumbani haswa kati katika
ya jiji . Katika hawa wateja wangu
kulikuwa na kijana mmoja
anayeitwa juma huyu juma
alikuwa na rafiki yake mmoja
anayeitwa Shy , kijana
mwembamba mwenye umbo la wastani , hana ndevu
halafu ni mcheshi sana ,
alifanikiwa kuiteka moyo
wangu , sasa nilitaka
kumwambia mara kibao
kwamba nimemzimia


Tatizo ni kwamba anayekuja
kunichukuwa pale ni juma ,
juma huja pale kwa
kusindikizwa na Shy , basi
juma akanitambulisha katika
website moja inayoitwa darhotwire
www.*****.com ,
nyumbani nikienda
kupumzika nilipenda
kushinda katika tovuti hii
kuchat na marafiki na watu wengine . Huyu shy nae nilimkuta katika
site hii usiku wa manane
anachat na jamaa zake , ila
siku moja nilikutana na
kijana mwingine anayeitwa
politeman , huyu ndio alinichanganya kabisa ,
kwanza jina lake na jinsi
aliyokuwa anaongea kweli
nilizimia mwenyewe bado
nikawa na siri kubwa moyoni
je hivi tukifanya ngono inakuwaje ?


Maisha yaliendelea tu , basi
nikimpenda politeman , huyu
kijana akawa anakuja mpaka
nyumbani kwangu wakati
mwingine na huwa nampa
computer yangu aitumie tukaenda zaidi nilimshitukia
kumbe huyu polite ana urafiki
wa kimapenzi na dada
mwingine anayeitwa salma
siku moja walipanga kwenda
kufanya mapenzi lakini polite akakataa ? Sikuamini macho yangu wala
masikio siku nyingi kama
naota kumbe polite alikuwa
na urafiki na dada mmoja
anaitwa Maria Chipz ??
Sikuamini , nilimuheshimu sana maria na sikutegemea
kama anaweza kufanya hivyo
hata siku moja , muda
ukaenda kumbe kuna dada
mwingine anaitwa REHEMA
naye alikuwa anampenda Politeman Miss upanga Naye
anampenda Politeman we
acha tu


Nikamwaga chini sikupenda
tabia zake za kitoto kitoto
anazowafanyia hao kina dada
wengine ingawa nilifanya
nae mapenzi kama mara 4
hivi na mara zote hatukutumia kinga na
nilikuwa nimeadhirika ila ni
siri yangu , polite hajui na
wengine wote hawajui lakini
ndio maisha hayo Haya ndio hivyo , nami sasa
hivi nakaribia kufariki dunia
niko zangu kitandani hapa
hospitali ya Amana mkoani
dar es salaam , kweli maisha
ni safari ishi upendavyo na sio watakavyo , mwisho wa yote
dunia sio hadaa wala dunia
haikuchukii au haitaki
kukufanyia chochote kibaya

Bali watu ndio hadaa , hata
kama ni ndugu yako rafiki
yako , hakikisha humpi nafasi
akutawale aweze kukumiliki
wewe na kukuamrisha
chochote kile anachotaka yeye , kama ukifanya hivyo
ndio utaishia kubaya kama
mimi Bosi wangu alinimiliki sana
nikampa penzi , kijana wa
mitaani nae alinimiliki
mpaka sasa nimeaona faida
zake na hasara za

Wacha ningoje siku zangu
nife nizikwe niende ahera


Kwaheri

USHAURI
SIKU ZOTE KATIKA HIZI
CHATROOMS ZA INTERNET
USIWE NA URAFIKI WA
KIMAPENZI NA MTU AMBAYE
HUMJUI KIUNDANI WENGI WANAKUWA NA WANAUME
AU WANAWAKE ZAIDI YA 1
NA WENGI
WANAAMBUKIZANA
MAGONJWA NA KUPEANA
MATATIZO SANA INA UMA SANA
    
Prepared By ABUU MAUTUNDU

No comments:

Post a Comment