Blogger Widgets

October 18, 2012

Huyu Ndio Mtoto Yatima alieungua moto Uso Mzima.

Click “Jion This Site” uwe MEMBER of FOL CLASSIC

MTOTO yatima, Juliana Inuka, mkazi wa Kijiji cha Mavanga wilayani Ludewa, mkoani Njombe ameungua vibaya usoni baada ya kuangukia moto.
 
Mtoto yatima, Juliana Inuka
 mtoto huyo katika kijiji hicho akiwa katika hali mbaya na alielezwa na wananchi kuwa aliungua zaidi ya mwezi mmoja uliopita na hakuwa anapatiwa matibabu kutokana na hali ya ufukara wa mtu anayeishi naye.
Hata hivyo, mwandishi huyo alifanya jitihada za ziada kwa kuchangisha michango ya fedha na kufanikiwa kumfikisha Juliana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako anapatiwa matibabu.
Akizungumza ,Mwandishi Godwin alisema aliambiwa kuwa mtoto huyo ana ugonjwa wa kifafa, hivyo siku ya tukio ambayo hakuweza kuikumbuka aliangukia moto uliosababisha aungue usoni na mbaya zaidi alikaa nyumbani miezi saba bila kupata matibabu.
“Kuna baadhi ya watu vijijini wana hali mbaya sana, kielelezo tosha ni huyu mtoto ambaye ameungua vibaya, nawashukuru sana wasamaria wema waliomchangia na kutuwezesha kumfikisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako sasa hali yake inaridhisha kidogo baada ya kupata tiba,” alisema Godwin.
Alitoa wito kwa watu walioguswa na habari ya mtoto huyu kuendelea kumchangia ili kunusuru maisha yake kwa kutuma michango yao kwa njia ya M- Pesa namba 0754026299 au Tigo Pesa 0712 750199 ambazo ni za mwandishi huyo anayeratibu matibabu yake.