Blogger Widgets

November 8, 2012

Ile Dawa ya kuwanatisha watu wanaotoka nje ya ndoa sasa yafika ndani ya jiji na yajidhihilisha ndani ya Temeke.


Shiliningi milioni 5 za kitanzania zinahitajika ili kuwanusuru watu wawili walionasiana wakivunja amri sita.

Watu wawili wakazi wa jijini Dar es Salaam wanadaiwa kukutwa wakiwa wamenasana wakati wakifanya tendo maalum la watu walio katika mahusiano (mke na mume) na kwakua wao sio mke na mume halali wamenasiana. 

Mume wa mwanake ambae amefikwa na maswaibu hayo ya mwaka jijini Dar es Salaam anahitaji kiasi hicho cha fedha ili atoe PASSWORD ya pin hiyo kali aliuyoiweka katika eneo takatifu la unyumba wao.


 Taarifa za awali kutoka Temeke zinapasha kuwa wawili hao wapo katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa unasuaji ambao wadadisi wa mambo hasa ya kijamii wanadai Hospitali hawataweza kuwanasua isipokuwa kwa wataalm wa jadi hasa Mume wa Mwenye mke ambaye aliwekewa tego. 

Blog hii itatujuza zaidi juu ya tukio hilo ambalo hadi sasa limekuwa ni gumzo jijini na kujaza umati mkubwa wa watu na kusababisha polisi kutumia mabomu ya machozi kutawanya watu eneo la tukio.   

UMATI wa watu wakiwa wamefurika katika Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam , mapema leo wakiwa na hamu ya kutaka kuwaona mwanaume na mke wa mtu waliodaiwa kugandiana wakifanya mapenzi katika moja ya nyumba za kulala wageni wilayani Temeke. 
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dk. Aman Malima akishangaa kuona umati huo
Police walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliofurika Hospitali ya  Temeke kushudia tukio hilo
Baadhi ya watu wakiwa hapo kushudia watu hao walio gandiana
Wananchi wakishinikiza waoneshwe wapenzi hao