Kukeketwa (Female Genital Mutilation).
Kukeketwa
ni kitendo cha kukata sehemu ya uke hasa kisimi kwa wanawake. Katika
Afrika kuna nchi 28 ambazo hufanya hicho kitendo cha kikatili, na pia
nchi kama Yemen na Indonesia bado wanafanya.
Ingawa
wanawake waliokeketwa huweza kurudia hali ya kuweza kufika kileleni,
walio wengi huathiriwa sana na hiki kitendo na kuwasababishia
kushindwa kufika kieleleni.
Kuna
baadhi ya mitazamo na malezi ya dini, jadi au tamaduni huwapa
wanawake mtazamo mbaya, finyu na usio na maana kuhusiana na tendo la
ndoa.
Katika
dini, jadi, na tamaduni nyingi ukiacha jando na unyago, elimu ya
mwanamke kuhusu mwili na uzazi havifundishwa wala kutamkwa matokeo yake
wanawake wengi hawaijui miili yao, kiasi ambacho unakuta kijana wa
kiume anamuoa binti hajui chochote kuhusu mwili wa huyo mwanamke na
mwanamke mwenyewe hajui chochote kuhusu mwili wake mwenyewe, akiguswa
chuchu anakataa kwani ni kwa ajili ya mtoto, hapo utategemea afikishwa
kileleni kweli?
Kisaikolojia.
Hili huchangia kwa asilimia 95 kwa matatizo yote yanayosababisha mwanamke asifike kileleni.
Adui mkubwa anayetisha sana wa mwanamke kutofika kileleni ni akili (mind.)
Hofu
labda ya kuachwa, mashaka, kutojiamini, kukasirika, donge moyoni,
kisirani au mahusiano kutokuwa mazuri huweza kusababisha mwanamke
kutofika kileleni, Kushindwa ku- concentrate kwenye tendo lenyewe na
kupata hisia halisi (sensations).
Kuwa
na mawazo ya kitu kingine wakati wa tendo la ndoa Mawazo hasi
(Negative) kuhusu tendo la ndoa, pia Kuwa mchomvu kutamfanya mwanamke
asifike kileleni.
Kibailojia
Kama
vile kuwa na mfumo ovyo wa mzunguko wa damu kwenye maeneo ya viungo
vya uzazi pia huchangia. Anaweza kuwa na uvimbe au kisukari pia
huchangia. pia hitilafu za viungo baada ya kufanyiwa upasuaji hasa
sehemu ya uke.
Umri (Menopause)
Kuna
wakati mwanamke kuanzia miaka 48 – 52 hupata mabadiliko ya upungufu
wa homoni na huo upungufu husababisha sehemu ya uke kuwa kavu wakati
wa tendo la ndoa.
Kuwa na uke mkavu huchangia katika ufanisi wa tendo la ndoa kuwa mdogo na hatimaye kushindwa kufika kileleni.
Si
kweli kwamba mwanamke akizeeka uwezo wa tendo la ndoa unakuwa mdogo,
muhimu ni kutumia vilainisho kama gel au KY jelly na libeneke
linaendelea kama kawaida.
Kutumia madawa (Medicaments).
kama
unatumia dawa za kuzuia msongo wa mawazo pia huchangia ile hamu ya
tendo la ndoa (libido) na matokeo yake kukosa kufika kileleni.
Pia
kuna dawa za uzazi wa mpango hupunguza hamu ya tendo la ndoa hasa
zile ambazo huingizwa mwilini (sindano). Pia dawa za kupunguza
pressure hupunguza uwezekano wa kufika kileleni.
Pombe,
madawa ya kulevya na sigara, Alkoholi na madawa ya kulevya hupunguza
sana hamu ya tendo la ndoa. Huathiri mfumo wa Fahamu unaohusika na
mzunguko wa hisia za mapenzi kati ya ubongo na uke.
Kama inavyoathiri (alkoholi) mwanaume kudindisha vilevile huathiri mwanamke kufika kileleni. Mwonekano, urembo na umaridadi:
Kwa mwanamke jinsi anavyoonekana na jinsi mwanaume anavyoonekana kuna sehemu katika hisia za mapenzi (emotions na feelings).
Kama
yeye mwenyewe anajijua kwamba hayupo vizuri kimwonekano (urembo,
usafi, harufu) na pia kama mwanaume hayupo sawasawa basi anakuwa
ameathirika sana kiasi ambacho hawezi kufika kileleni.
Pia
wanawake wana uwezo mkubwa kunusa harufu kuliko mwanaume hivyo harufu
yoyote mbaya kwake huwezi kumpeleka nje kabisa ya njia ya kwenda
kileleni.
Mazingira
Kama
eneo au chumba mlichopo hakina usalama kama vile anahisi mtu
anachungulia au anaweza kuingia, kwa mwanamke hiyo ni issue kwani hawezi
kufika kileleni kwa sababu ya usalama wake.
Je kuna jinsi ya kuondoa tatizo la kutofika kileleni?
Kujiruhusu mwenyewe kupenda tendo la ndoa na zaidi kupenda kufika kileleni kwa hamu kubwa.
Kuwa responsible kwa mambo yote yanayohusu ufanisi wa tendo la ndoa.
Kujipa
elimu na maarifa kuhusu elimu ya mapenzi kwa mwanaume na mwanamke,
viungo vinavyohusika na kila kitu kinachiweza kukupa tofauti katika
ufanisi uimarishaji wa tendo la ndoa kama unavyosoma hapa sasa hivi.
Kuwa na mawasiliano wakati wa tendo la ndoa hasa kuhusiana na maeneo yote ambayo unasisimka pale ukiguswa au kuchezewa.
Kufanyia kazi kila tatizo lolote la kisaikolojia na kupata solution kabla ya tendo la ndoa.