Blogger Widgets

January 17, 2013

Kumbe kuna Ushindani Kati ya Bongo Movies na Bongo Fleva,Upande Upi wengi "wanapush Ndinga Kali"(Magari ya Kifahari)

TAMBO za mastaa kumiliki mikoko ya kifahari linazidi kuchukuwa nafasi kubwa katika tasnia tofauti za burudani Bongo.
Amani linakuanikia upinzani wa mikoko ya mastaa wanaoigiza filamu na wale wanaoimba muziki wa Bongo Fleva.

Bongo Movies
Listi inaongozwa na Vincent Kigos ‘Ray’ anayesukuma Toyota Lexus lenye thamani ya Shilingi milioni 60 za Kibongo kama aliyokuwa akimiliki marehemu Steven Kanumba.
Wapo kina Jacob Steven ‘JB’ anayesukuma Verosa, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ (Mark-X) na Jacqueline Wolper (Toyota Brevis).
Wengine ni Jenefer Kyaka ‘Odama’ (Harrier), Aunt Ezekiel (Voxy), Steve Mangere ‘Steve Nyerere’ (Verosa),
William Mtitu (Toyota Oppah).


Bongo Fleva
Listi inaongozwa na Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ (Nissan Murrano) lenye thamani ya shilingi milioni 70, linatajwa kulipiku Lexus ya Ray.
Wengine ni kina Diamond (Prado) Dully Sykes (GX110 Mark 11), Jafarai (Harrier), H-Baba (Nissan X-Trail) Marlaw (Mercedes) na Ally Kiba (Honda).
NANI MSHINDI?
Kutokana na baadhi ya mastaa ambao wameorodheswa hapo juu, tathmini inaonesha Bongo Fleva inaongoza kwani Lady Jay Dee ndiye anamfunika Ray ambaye anatajwa kuwa katika nafasi za juu kwa upande wa Bongo Movies.

WAPO KIBAO HAWAJAJITANGAZA!

Nayatambua magari mengi ya mastaa ambao kwa namna moja au nyingine hayakuweza kuiingia kwenye listi hii kutokana na ufinyu wa nafasi.
Wakati mwingine, tutayachambua magari mengine ya mastaa wengine.


GPL