Blogger Widgets

February 17, 2013

Alichokisema Linex Kuhusu Mpenzi wake Mzungu"Suzi' na matatizo yaliyomkuta mpaka Kufikia Hatua ya Kuachwa

 
Linex akiwa na shemeji yetu "Suvi" kushoto

 Kama unakumbuka vizuri, miezi kadhaa iliyopita, baada ya kuandikwa kwenye  magazeti ya udaku kuwa anamsichana mwingine, na yeye kuruka futi mia na kusema bado yupo na mpenzi wake wa kizungu "Suvi" ambae ndio kila kitu kwake, leo hii Linex amethibitisha kuwa mambo yao hakuna anaeweza kuyaingilia..ukimsikiliza kwa makini utagundua kuwa anajiami sana kwa mpenzi wake huyo na ndo maana anajaribu kukuambia kuwa atakua ana matatizo kama kuna kvuvi atakae weza kutupa nyavu baharini na kumvua mpenzi wake wa sasa.

"kama kuna mvuvi atatupa nyavu kumvua huyu shemeji yenu wa sasa hivi basi ntakua nna tatizo, kwasababu maisha yangu mengi, nafkiri labda kwa sababu ya the way i was living, sababu unajua mi ntaokea mtaani sasa labda the way nilivyokuwa naishi ilikua

inafikia point watoto wa kike wanachoka maisha yangu ya mtaani na nini,  so wanaamua kunichoka na wanaamua kuniacha na kuanza na maisha mengine, so hakuna jambo jipya kwenye swala la kupenda k wangu mimi yaani ...mi sina kinyongo na mvuvi ambae atatupa nyavu baharini atafanikisha kumvua samaki ambae mi nilikua napenda kumuona aendelee kuwa baharini akifanya maswala yeke".