Blogger Widgets

February 28, 2013

Picha Tukio la Mtoto Mchanga aliesadikiwa Kuzaliwa Usiku wa Kuamkia Leo alieokotwa Kimara Baruti.HUU NI UKATILI


Wasamariawema wakimsafisha uchafu mtoto mchanga baada ya kumuokota  katika eneo la bondeni huko Kimara Baruti Bondeni karibu na maeneo ya Ubungo Kibangu.


Kitoto hicho baada ya kusafishwa na wasamaria wema 
 
Leo asubuhi wasamaria wema  wamekiokota kitoto kichanga cha kiume huko Kimara baruti  bondeni karibu na Ubungo kibangu , wasamaria hao baada ya kumsafisha uchafu na damu waliamua kumpeleka mtoto huyo kwenye hospital ya Palestina kwa huduma ya kwanza na baadae  Hospital ya Mwananyamala ambako kuna kitengo maalumu cha kuhudumia watoto wachanga . Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa kuna uwezekano wa mtoto huyo kutupwa leo asubuhi na hii imetokana na mtoto huyo  kukutwa akiwa hai na uwepo wa damu mbichi mwilini mwake
Respect:Chinga