WAUMINI ya dini ya Kikristu wamjia juu mtangazaji wa kipindi cha 'Talk Show' Opra Winfrey kwa kukosa uadilifu katika mtandao wake
Alionyesha kukosa uadilifu huo baada ya kuonyesha picha katika mtandao wake zinazomdharilisha mwanamke zinazoonyesha unyanyasaji, mateso na mambo ya mapenzi hadharani (mambo yanayofanyika kitandani wazi)
Mkurugenzi mtendaji wa Uadilifu katika vyombo vya habari Dawn Hawkins alisema mwanamke anatakiwa kupendwa kuheshimiwa na si kuchochea matendo maovu na unyanyasaji kwa wanawake kwani hali hiyo inaongeza unyonge wao
"Opra na mtandao wake wameonekana kukata tamaa kwa kuonyesha vitu ambavyo havipo katika maadili, unaweza kuona ni kama burudani kwa kuendeleza unyanyasaji majumbani hasa ya wanawake hivyo mimi ninavyodhani Opra lazima alipe dhidi ya unyonyaji" alisema Dawn Hawkins
Aliongezea kuwa Uadilifu katika tasnia ya habari unaamini kuwa wote wanawake, watoto na wanaume wana asili ya utu hivyo vipindi kama hivyo vinavyoonyesha udharirishaji, hali inayosababisha kualibu mahusiano ya afya pia uharibu mtazamo sahihi kiubinadamu