Blogger Widgets

April 16, 2013

Huu Ndio Ukweli Kuhusu Kuvunjika kwa Kundi la Camp Mula

CAMP MULLA

Ni wiki kadhaa sasa toka kuripotiwa kwa mara ya kwanza habari za kutengana kwa kundi la muziki kutoka nchini Kenya ambalo linafahamika kwa jina la 'Camp Mulla' huku mashabiki wake wakibaki njia panda wasijue nini kinaendelea ndani ya kundi hilo lililojizolea umaarufu duniani koke. Hata hivyo tayari wasanii wanaounda kundi hilo wamefunguka na kuweka wazi ukweli wa jambo hilo ili kuwatoa hofu mashabiki wao lukuki.

Wasanii hao wa miondoko ya Hip Hop wameelezea kuwa kutengana kwao haimaanishi ndio mwisho wao katika kufanya muziki, bali kila mmoja ameona ni bora ajishughulishe na project zake binafsi. Imeelezwa kuwa 'Taio Tripper, K'cous na Miss Karun' wanatarajia kuondoka nchini kwa ajili ya kujiendeleza zaidi na masomo wakati 'Shappaman' ataendelea kuwepo nchini Kenya na kuendelea kufanya shughuli zake za kimuziki

From: kizobrax