Blogger Widgets

April 16, 2013

Msanii wa Bongo Movie ajifungua Mtoto wa Kiume.Hongera!!

Msanii Davina
msanii wa filamu nchini tanzania Halima yahaya alimaarufu kama Davina amejifungua salama mtoto wa kiume mapema hii leo.

Akipiga stori muda mfupi na  thesupestarstz  msanii huyo mkali wa movie bongo movie ambapo mwandishi wetu alikuwa eneo la tukio  amesema anashukuru mungu kujifungua salama na hilo ndilo alilokuwa anamuomba mungu kila kukicha katika kipindi chote cha miezi tisa.


Divina ambaye yupo hosptali ya Aghakan alipojifungulia mtoto wake huyo amewashukuru pia mashabiki wake kwakuwa naye katika kipindi chote cha hali yake ya ujauzito hadi kufikia kujifungua salama mtoto huyo wa kiume


Hapa Davina Akiwa na Johari na Jack Wolper picha na maktaba yetu

 Hadi thesuperstarstz inaondoka eneo hilo wasanii kibao wa bongo movie na wa muziki walikuwa wanamiminika kuja kumpongeza msanii huyo mpole na mwenye

kupendwa sana na wasanii wenzake kwa wema na kujali,tunamtakia kila la kheri  na afya njema mtoto huyo na pia tunamtakia mama yake mapumziko mema afya njema

na kila kheri.