Blogger Widgets

April 20, 2013

Taarifa na Matukio ya Picha ya Kuawawa kwa Sajenti wa Polisi SALIM MTEPA Wilayani Kahama

MWILI WA MAREFEMU SALIM MTEPA UKIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA MUDA MCHACHE BAADA YA KUFARIKI.
MAREHEMU SALIM MTEPA ENZI ZA UHAI WAKE

 
MWILI WA MAREFEMU SALIM MTEPA UKIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA MUDA MCHACHE BAADA YA KUFARIKI.

HAPA MWILI WA MAREHEMU UKISHUSHWA NYUMBANI KWAKE MDA MCHACHE BAADA YA KUTOLEWA HOSPITALI
                               Jeneza lililobeba mwili wa Sajenti Mtepa

KAHAMA
Askari Polisi wa kitengo cha usalama Barabarani Salim Mtepa(41), ameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi kwenye kitongoji cha mhongolo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia leo.

Mkuu wa jeshi la polisi wilayani humo George Simba ameiambia redio Kahama fm kwamba marehemu Mtepa ameuawa, wakati akijaribu kuokoa mali iliyokuwa imeibiwa na vibaka kutoka kwenye duka lililoko nyumbani kwake.

Amefafanua kwamba, saa 9.30 usiku vibaka walienda kuvunja kwenye duka la Mtepa ambamo huwa inatunzwa pikipiki, na kwamba baada ya kuikosa walianza kubeba mifuko ya sukari na mchele kabla ya Mtepa ya kutoka nje.

Simba amesema, inadhaniwa kwamba, watu waliokuwa wamekuja Kahama kwa ajili ya machimbo ya dhahabu ya mwime ndio wanaotangatanga jinsi ya kupata nauli za kurudia kwao hadi kufanya uhalifu kama huo.

Amewaomba watu wenye taarifa za wauaji hao watoe taarifa kwa siri polisi ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwani wanataka kuharibu sifa ya Kahama yenye watu wanaopenda utulivu na amani.

Simba amesisitiza wananchi wawe makini na watu wasiowaelewa vizuri kukaa nao nyumbani kwani ndio wanaogeuka na kuanza kuhatarisha maisha ya wananchi wasio na hatia.

Marehemu Mtepa amefariki wakati anapatiwa matibabu Hospitali ya wilaya ya Kahama na kwamba mwili wake umesafirishwa leo kwenda Dar-es-Salaam kwa mazishi.

MATUKIO KATIKA PICHA

MKUU WA KITUO CHA POLISI ISAKA MR THOMAS KATIKATI YAKIWA NA VIONGOZI WALIOTEULIWA KUKUSANYA RAMBIRAMBI WAKIPITIA MAJINA YA MICHANGO

MDOGO WA MAREHE KATIKATI AKIFARIJIWA NA NDUGU NA JAMAA

MKUU WA KITUO CHA POLISI KAHAMA OCD GERGE SIMBA KULIA AKIWA NA MKUU WA KITUO CHA POLISI ISAKA MR THOMAS AKIWA NA KIONGOZI WA KIISLAMU WAKIPITIA RATIBA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU,

KIONGOZI WA KIISLAMU AKITOA MAELEKEZO YA KUUGA MWILI WA MAREHEMU.

SHEKHE MKUU WA WILAYA YA KAHAM OMARY DAMKA AKITOA DUA YA KUUGA MWILI WA MAREHEMU.

WATU WAKIWA NA SURA YA MAJONZI KATIKA MSIBA HUO.

VIONGOZI WA POLISI WAKIWA KATIKA SURA ZA MAJONZI KATIKA MSIBA HUO.

MKUU WA KITUO CHA POLISI ISAKA MR.THOMAS AKITOA WOSIA KWA WATU WALIOHUDHURIA MSIBA HUO.

HALI YA TAFRANI ILITOKEA KATIKA MSIBA HUO BAADA YA NYOKA KUIBUKA KATIKATI YA UMATI WA WATU NA HATIMAYE KULIWA.

MKUU WA KITUO CHA POLISI KAHAMA OCD GEORGE SIMBA AKISOMA HISTORIA YA MAREHEMU

KINA MAMA WAKIWA KATIKA SURA ZA MAJONZI

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA MH BENSON MPESYA AKIWASILI KATIKA MSIBA HUO.

KIONGOZI WA UMOJA WA WAENDESHA PIKIPIKI IDDY SAM MAPANDE AKITOA NENO KWA NIABA YA MADREVA BODABODA WA WILAYA YA KAHAMA.
IDDY SAM MAPANDE AKITOA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA KITUO CHA POLISI KAHAM OCD GEORGE SIMBA.

MAJONZI NA SIMANZI.

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA BENSON MPESYA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WALIOHUDHURIA KATIKA MSIBA HUO.

MASHEHE WA WILAYA YA KAHAMA WAKIWA KATIKA MSIBA HUO.

MWANANZENGO AKIZUNGUMAZA KWA NIABA YA WANANCHI WA KIJIJI HICHO.

KAMANDA THOMAS AKISOMA MAJINA NA KUTOA SHUKRANI KWA WATU WALIOCHANGIA MSIBA HUO.

KAIMU KAMANDA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ONESMO LYANGA AKISALIMIANA NA MKUU WA WILAYA YA KAHAMA MUDA MCHACHE BAADA YA KUWASILI KATIKA MSIBA HUO.

OCD SIMBA KULIA AKIMKARIBISHA KAIMU KAMANDA MKUU WA MKOA ONESMO LYANGA KUZUNGUMZA NA WANANCHI.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA SHINYANGA ONESMO LYANGA AKIZUNGUMZA NA WANACHI WALIOHUDHURIA KATIKA MSIBA HUO HUKU AKIHAIDI KUWATIA MBARONI WALIOHUSIKA NA TUKIO HILO.

KINA MAMA WAKIWA KATIKA MSIBA HUO.

SHEHE AKIOMBA DUA YA KUMUOMBEA MAREHEMU.

WATU WAKIWA KATIKA DUA YA MWISHO YA KUUOMBEA MWILI WA MAREHEMU.


MAMA WA MAREHEMU SALIM AKIWA ANATOKA NDANI KWENDA KUANDA GARI KUELEKEA JIJINI DAR ES SALAAM

SAFARI YA KWENDA JIJINI DAR ES SALAAM

MAJIRANI WALIOTEULIWA KUMSINDIKIZA MKE WA MAREHEMU WAKIELEKEA KUPANDA GARI.

DADA WA MAREHEMU AKIWA HOI KWA KILIO AKIAIDIWA KWENDA KUPANDA GARI

ASKARI WA KIKOSI CHA ZIMA MOTO WAKIWA KATIKAMSIBA HUO


MWILI WA MAREHEMU UKITOLEWA NDANI TAYARI KWA SAFARI YA KUUELEKEA DAR ES SALAAM.

WANANCHI WAKISAIDIZANA KUBEBA JENEZA KUPELEKA KWENYE GARI.

MWILI WA MAREHEMU AKIPELEKWA KWENYEGARI.

GARI IKIWA TAYARI KUPAKIA MWILI WA MAREHEMU.

WANANCHI WAKIWA NJEE KUUAGA NA KUUSINDIKIZA MWILI WA MAREHEMU.

UMATI WA WATU WALIOKUWEPO KATIKA MSIBA HUO.

MOJA YA GARI ILIYOTOLEWA NA NDUGU NA MARAFIKI KWA AJILI YA KWENDA DSM.

MKE WA MAREHEMU AKILETWA KWENYE GARI.

MKE WA MAREHEMU ALIYEJIFUNIKA NGUO ZA BLUE AKIJIANDAA KUPANDA KWENYE GARI.

SAFARI IKIANZA KUELEKEA JIJINI DAR ES SALAAM

ASKARI POLISI WA KAHAMA WAKIWA KATIKA GARI KUUSINDIKIZA MWILI WA MAREHEMU.

SAFARI YA DSM


GARI ILOBEBA MWILI WA MAREHEMU IKIANZA SAFARI YA KUELEKEA DAR ES SALAM
MADREVA BODA BODA WAKIONGOZA MSAFARA KUSINDIKIZA MWILI WA MAREHEMU.
 
From:KB BLOG