Blogger Widgets

May 26, 2013

Endelea na Simulizi ya HATOOLEWA KAMWE sehemu ya Pili Chini ya Utunzi wa ABDULMALIK SIRAJSEHEMU YA PILI
Mtunzi: ABDULMALIK SIRAJ
 Simulizi:NA HATOOLEWA KAMWE
********************

Mzee Kiashama alijikuta anakuwa mlevi wa kupindukia kutokana na kukosa mtoto kwasababu ya matatizo ya mimba kuharibikia tumboni aliyokuwa nayo mke wake Eliza.Siku moja mwanamke Eliza alikua akifagia uwanja unaozunguka nyumba yao ambapo pembeni kidogo ya mlango alikuwepo Mzee Kyashama akirekebisha sturi kwakuigongelea misumali zaidi ili iimalike.Ndipo Mke Wake Eliza alianza kujihisi kama anataka kutapika naghafla akaanza kukimbia kama kibelenge kuelekea kando kidogo ya nyumba na kuanza kutapika huku ameinamisha mgongo wake pamoja na kichwa Huku mkono ukibaki kifuani!.jambo hilo lilimshtua mzee kyashama naye akainuka harakaharaka na kutupa nyundo chini na kuanza kutembea kwa hatua ndefundefu na za harakaharaka huku akitweta kuelekea pale mke wake alipojiinamia..akamfikia na kuanza kumuuliza unatatizo gani mke wangu huku akihemea juujuu akiwa amemshika mgongoni..mke wake hakumjibu bhali alizidi kutoa mafundo ya matapishi kutoka mdomoni mwake uku akizidi kulegea kwa kukosa nguvu!..hali hiyo ilizidi kumtia kiwewe mzee kwa hofu kwamba huwenda akaja kumkosa mke wake kipenzi..palepale akajawa na wazo la kukimbia kuelekea ndani na kurudi akiwa amebeba jagi lenye maji kiasi na kuanza kumuhudumia mke wake kipenzi..ambapo mwanamke Eliza alikunywa yale maji na mengine akayatumia kusukutua mdomoni kisha kuyatema!..mzee kyashama alimkokota mkewe taratibu mpaka alipomfikisha chumbani na kumlaza kitandani huku akimpepea kwa kutumia mfuniko wa Plastiki..taratibu mpaka mke Wake  Eliza akachukuliwa na usingizi..baada ya kama nusu saa Eliza alishtuka kutoka usingizin na kugundua kuwa mme wake amekaa pembeni ya kitanda chake huku akimuangalia kwa huruma...ndipo mzee kyashama akamshika kwenye paji la uso nakumuuliza kiutaratibu kwa sauti ya chini ''vipi mke wangu unaendelaje?''. Eliza naye akajibu kiutaratibu ''naendelea vizuri mume wangu ila kuna kitu nataka nikufahamishe!''..ukimya mfupi ukatawala,mzee kyashama akabadisha mkao na kumgeukia akiwa amemuangalia usoni kwa makini kisha akamwambia ''ondoa hofu mke wangu ongea chochote mkewangu kwamoyo mkunjufu nitakipokea!!

****************

Mwanamke Eliza aliinua uso wake na kumuangali mumewe usoni kisha akamwambia ''MUME WANGU NINA UJAUZITO'' hizo taarifa hazikumshangaza mzee kyashama sana sana zilimuongezea mawazo akijua kuwa hata hiyo mimba itaporomoka kama nyingine.. Bi Eliza baada ya kutoa habari hiyo alionekana amepooza kama yuko kwenye dimbwi la mawazo mazito akanyong'onyea mithili ya mlenda..ndio mzee kyashama akamsogelea na kumkumbatia kwanguvu huku akimliwaza kwa kumwambia kiutaratibu kabisa..''mke wangu usiwaze sana yote ni mipango ya Mungu naomba usikate tamaa mke wangu pengine huyu ndio atakuja kuwa shujaa wetu''..maneno yale yalizidi kumuongezea Uchungu mara akaangua kilio kitakatifu huku akibubujikwa na machozi kama mtoto mdogo...jambo hilo pia lilizidi kumuuzunisha mzee kyashama kulengwalengwa na machoz katika macho yake ila hakuacha kumkumbatia mke wake kipenzi mpaka alichotwa tena na usingizin akasinzia..mzee kyashama akamlaza kitandani na kumfunika na shuka kiustadi kabisa.,alipomaliza hayo alitoka nje na kwenda kumuandalia chakula mkewe..

BAADA YA MIEZI MITANO(5)
Mzee kyashama alioneka ni mtu mwenye furaha kupita kiasi hasa pale alipokuwa akilitazama tumbo kubwa la mkewe alioneka akicheka na kutabasamu muda wote..mzee kyashama akaacha kabisa kwenda kilabuni muda wote alishinda nyumbani akimuhudumia mkewe kwa kufanya kazi zote za nyumbani ikiwemo kupika,kufua na kuosha vyombo..haikuwa kawaida kwa Bi Eliza kutunza mimba mpaka ikafikia miezi 7 mimba zake zote zimekua zikiharibika pindi tu zifikishapo miezi minne au mitano..jambo hili Lilimjaza imani na furaha isiyo na kifani ambayo aliidhihirisha kwa kutembea maeneo tofauti tofauti huku kitumbo mbele ili watu wamuone na wamsifie..kwakwel ilifika miezi nane tumbo la mwanamke eliza liliongezeka na kuwa kubwa sana mithili ya pipa jambo lililowafanya watu wote waamini kwamba Bi Eliza ana mimba ya mapacha mpaka wakambadilisha jina na kuanza kumuita MAMA BALONGO!... **** Miezi tisa ikafika Bi Eliza alifanikiwa kujifungua kitoto chenye afya nzuri na chenye kupendeza sana katika hospitali ya GOVERNMENT iliopo bukoba mjini...punde  tuu baada ya Mzee kyashama kuingia wodini zilisikika shamlashamla za mzozo mkubwa mabishano ya hali ya juu pamoja na kelele ikabidi manesi waingilie kati mzozo huo ambao ulikuwa ni baina ya Mzee kyashama pamoja na Bi Eliza....