Blogger Widgets

May 25, 2013

Hapa Ndio Wema Sepetu Alifikia Kwenye Mapenzi Yake


HABARI zinasema kwamba staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, ‘Beautiful Onyinye’ ameongeza idadi ya wanaume katika uhusiano wake na kuzidi kuwa katika chati ya magazeti ya Bongo.
 
 
Wema ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Endless Fame, anadaiwa kuwa beneti na kijana aitwaye Robby lakini mwenyewe amesema kwamba hakuna anayeweza kumtenganisha na wanaume.
Habari zinasema kuwa, Wema na Robby wamekuwa wakipiga picha za kimahaba na mnyange huyo kuziingiza kwenye mtandoa wake na kumtambulisha kijana huyo kwa jina la ‘Honey’

Mei 22 mwaka huu, mwandishi alifika ofisini kwa mrembo huyo, Mwananyamala Komakoma jijini Dar es salaam na kumbana kwa maswali juu ya kuvuja kwa picha zake hizo akiwa na Robby na nyingine akiwa na wanaume wengine tofauti.
“Watu wamekuwa wakinizungumzia kila kukicha, tena maongezi yao yamekuwa yakianzia kwenye baadhi ya picha zangu, kila mtu ana namna ya kutengeneza ‘laifu’ yake na miye huwa sioni shida mwanaume asiye hawara yangu kunikisi au miye kumkisi,” alianza kujitetea.
 
“Ukifuatilia historia yangu mara nyingi utagundua marafiki zangu wengi ni wanaume kuliko wanawake na wengi wao wanakuja kwangu, tunakunywa na wanaondoka mida mibovu, kwa asiyenijua anaweza kuhisi ni mabwana zangu kumbe siyo, hata kwenye mitandao huwa sioni tabu kuweka picha za mtu akinikisi au nikimkisi,” aliendelea kusema.
“Siwezi kubadilika hii ni life style yangu. Siwezi kuacha kuwa karibu na marafiki wa kiume, hivyo ndivyo nilivyoumbwa watu wasinishangae, suala la kukutana na mtu na kupiga naye picha siyo ishu kwangu, ningekuwa mtu wa ajabu sana kama ningekuwa nawakisi midomoni au wao kunikisi mdomoni,” aliongeza.
Wema amesema kuwa watu wana hisia mbaya juu yake na Robby jambo ambalo siyo sahihi kwa kuwa, katika maisha yake anawapenda marafiki wa kiume zaidi ya wanawake.