Blogger Widgets

May 18, 2013

Hawa Ndio Maqueen Wanne wa Bongo wanosadikiwa Mmoja wao Kuingia Big Brother

Jack PentezelKwa mujibu wa 
chanzo chetu (tunaficha jina lake), 
mastaa hao wa kike, mmoja 
ndiye ataibuka mshiriki kwa
 mwaka huu ambapo atakaa 
ndani ya mjengo kuanzia 
Mei 26, 2013 ambapo 
shindano litaanza rasmi. 

Jack Patrick“Mimi nawamegea 
tu kwamba kati ya Wema, 
Baby Madaha, Jack wa Chuz
 na Jack Patrick mmoja wao
 anakwenda Big Brother mwaka huu.
Wema sepetu“Halafu
 ninachojua mimi, mshiriki
 ameshatumiwa taarifa kutoka 
Multi Choice, ila tatizo
 wale jamaa wanataka mtu 
msiri sana, mshiriki hatakiwi 
kumwambia mtu mpaka siku 
atakapoondoka,” kilisema chanzo chetu.
Risasi Jumamosi lilipiga 
kiguu hadi Ofisi za Multi Choice
 jijini Dar na kuulizia
 Mbongo anayekwenda, 
likakumbana na majibu haya:


Baby Madaha“Sisi pia hatujui. 
Unajua ilivyo ni kwamba huwa
 tunatuma majina, sifa na 
anuani za watu kama watano
 kule Sauzi, halafu wao 
wanaangalia vigezo vyao, 
anayeshinda anataarifiwa
 kutoka kulekule bila sisi 
kujua,” alisema mtumishi mmoja
 ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.
Risasi Jumamosi juzi Alhamisi
 liliongea na Jack wa Chuz
 ambaye alisema aliwahi 
 kuombwa kushiriki shindano
 hilo kwa sababu ya ushombe 
wake lakini hakuweka wazi
 kama alijaza fomu za maombi au la!
Aidha, Baby Madaha alipoulizwa 
alikiri kujaza fomu za 
kukusudia kushiriki siku za nyuma 
akiwa sambamba na Wema
 lakini akasema hajui nani
 kashinda ingawa lazima
 mshiriki ameshapatikana kati yao.
“Nasikia mshiriki anatakiwa
 kujijua wiki tatu au mbili kabla. 
Kwa hiyo atakuwa tayari anajijua,
 inakuwa siri ya mtu, hakuna 
anayeweza kujitaja kwa watu,”
 alisema Baby Madaha.
Simu ya Jack Patrick haikuwa 
hewani siku hiyo huku watu wake wa karibu wakisema yupo nje ya Bongo
 kibiashara zaidi. Simu ya 
Wema muda mwingi iliita 
bila kupokelewa hadi mpigaji akachoka.
Kwa upande wa wanaume, 
wanaotajwa kushiriki shindano 
hilo mwaka huu ni staa wa 
sinema za Bongo, Hemed 
Suleiman ‘PHD’, nyota wa 
Bongo Fleva, Khaleed Mohamed 
‘TID’ na aliyewahi kuwa 
Mtangazaji wa Clouds TV,
 Rommy Jones ambaye ni 
ndugu na Mbongo Fleva, 
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
From:GPL