Blogger Widgets

May 23, 2013

Hii Hapa Sasa Ile Simulizi ya Kusisimua "NA HATOOLEWA KAMWE" Sehemu ya KWANZA Simuliz:NA HATOOLEWA KAMWE
 Mtunzi: ABDULMALIK SIRAJ
Sehemu Ya: KWANZA
****************


Ilikuwa siku ya juma nne asubuh mida ya saa tano mnamo tarehe 7/5/2013 nikafunga safar kuelekea kwa jiran yangu maeneo ya tandale kwa tumbo aitwae BIBI KUNUKA nipokaribia mlangon
i kwake niliskia harufu kali sana ikitekenya pua zangu ila ikabidi nipige moyo konde na kujongea karibu kabisa na mlango na nikaanza kubisha hodi...hodii hodii (gongongong)...nilibisha zaidi ya dakika kumi hama bibi hajazoea wageni mara nikaona mlango ukifunguliwa chuiiii ...hapo ndo harufu ya uvundo na maharagwe yalichacha ikatia fola hata bila kuuliza nikawa nishafahamu sababu za yeye kuitwa Bibi kunuka...mlango ulipofunguliwa nikaona sura bibikizee ikitoa macho kwamshangao!..ndipo nikakohoa kidogo kisha nikamsalimia ''Shikamoo bibi''..bibi akiwa ananiangalia kwa makini kama vile ananifananisha akaniitikia ''Marhaba mjukuu wangu''...akanambia wewe sio mgeni machoni mwangu wewe si mtoto wa mwenyekiti!?...nikacheka kidogo..nikamwambia bibi mimi sio mtoto wa mwenyekiti mimi jiran yako kila mara nakukuta hapa nje umekaa nakusalia...bibi akasema uzee nao huu...kimya kifupi kikatawala  nikawa bado nimesimama nje ndipo bibi akasema...mjukuu wangu ngoja nikuletee mkeka ukiingia ndan kwangu utaugua mafua kuna harufu kali!..ngoja nikuletee mkeka tukae wote hapa nje!...bibi akaingia ndani punde tu akarudi na mkeka ulochakaa sana kwa matobo na viraka kibao!...tulipo kaa chini nikamkabidhi mfuko wa nailon ambamo ndani yake palikuwemo chapati mbili na soda ya kopo...bibi alipofungua mfuko na kuona vilivyomo nikamuona anachukua chapati harakaharaka nakaishambulia mara akaanza kukuhoa chapat imemniga anatapatapa kama anataka kukata roho...kuona hali hile mimi nikaogopa nikaifungua soda nikamnywesha...akainywa kwa fujo na yenyewe ikampalia ngoja aanze kutapika sasa!..bibi katapika vitu havieleweki vina rangi ya kijani nikaogopa huku kichwani nikijiuliza huyu bibi alikua anakula majan ya mbuz au...baadae nikahisi labda ndo nyongo kama watu wanavyosema kutapika nyongo...ikabidi niingie ndan kumtafutia maji ya kunywa...lalalala nilikuta harufu iyo ndani hakueleweki kumbe ule mkeka ndo huwa analalia hana kitanda wala godoro nikachota maji kwenye mtungi nikampelekea...akanywa maji akatulia kwa muda...kisha akaniuliza ulikua unashida gani kijana?


***********************


Nikamjibu!...Bibi mimi ni mwandishi wa simulizi kama tamthilia pamoja na riwaya!!..akaniuliza kwahiyo ulitaka nikusaidie nini?..akaniuliza!..nikamwambia kabla ya yote bibi naomba nikuulize!..kwaunyonge akanijibu...uliza tu mjukuu wangu!...nikamuuliza..''bibi mbona unaishi pekea yako tena kwa tabu sana kwani watoto na wajukuu wako wapi?''..nilimuona bibi kajiinamia kama anatafakari akanigeukia kuniangalia..ndipo nilipo gundua kuwa macho yamebadilika na kuwa mekundu utadhan amevuta bangi au msubah...nikaogopa ukunikijiuliza..huyu bibi ni mchawi kweli au watu wanamsingizia..mara akajiinamia na kuangua kilio..mpaka wapita njia walikua wakiniuliza!..umemfanyaje bibi yako?..sikuwajibu nilibaki kimya mpaka bibi alipo maliza kulia na kutulia kisha akaniambia mjukuu nashindwa nianzie wapi ...kiufupi mimi ndo mjukuu mimi ndo mtoto navilevile mimi bibi....alipomaliza kuyaongea hayo kwa unyonge akawa kimya kwa muuda kisha nikamuuliza...''bibi jina lako kamili unaitwa nani!?..akanitazama uson kisha akanijibu..''jina langu kamili naitwa SUZANA PATRICK..nimtoto wa kwanza wa marehem Mzee Patrick ila baba yangu huyo alijulikana zaidi kama Mzee Kyashama...!


********************MZEE KYASHAMA/MZEE PATRICK,ni mzee aliyekuwa anaishi na mke wake aitwae Elizabeth...mzee kyashama/mzee patrick alijishughulisha zaidi na ufundi selemara huku mke wake akijiusisha na kilimo kwenye mashamba ya wazungu...ukimya na upweke ulitawala zaid ndan ya nyumba ya mzee patrick kutoka na kutokufanikiwa kupata mtoto ndani ya nyumba ambaye kila mimba aliyokuwa akiipata ilikuwa ikiharibikia tumboni jambo hilo liliwatia simanzi mpaka wakaanza kuamini kuwa wamechezewa nakuanza kuzunguka kwa waganga wa kienyeji tofautitofauti...ila bado juhudi zao hazikuzaa matunda ukizingatia wamepoteza pesa na muda mwingi kushughulikia hilo swala...mzee patrick alikuwa anampenda sana mke wake hivo hakutaka kuoa mke mwingine...kutokana na mawazo mzee patrick kyaruz alijikuta anakuwa mlevi wa kupindukia...na kila alipokuwa akilewa alikuwa anapayuka maneno barabara nzima...kutokana na tabia yake ya kuachama achama watu wakambatiza jina la MZEE KYASHAMA na jina hilo likamshika mpaka akaamua kulikubali!.....