Blogger Widgets

May 29, 2013

Hili Ndio Tatizo Lililompata Agness Masogange na Kusababisha Atoke Usiku Mbio na Night Dress Akiwa Peku

             

Maajabu Agness Jerald ‘Masogange’ anasumbuliwa na tatizo la kuota ndoto mbaya usiku na kuamka kisha kutoka nje na kutimua mbio.


VIDEO Queen wa Bongo Fleva, Agness Jerald ‘Masogange’ anasumbuliwa na tatizo la kuota ndoto mbaya usiku na kuamka kisha kutoka nje na kutimua mbio, jambo ambalo kwa wengi linaweza kuonekana kuwa ni maajabu.
 
                                                        Agness Jerald ‘Masogange’.
Habari kutoka kwa sosi wetu, zinasema kuwa katikati ya wiki iliyopita, Masogange akiwa ndotoni, aliamka na kufungua milango na geti la nje kisha kutimua mbio umbali mrefu akiwa na nguo za kulalia na miguuni hana  viatu.


“Bahati nzuri ni kwamba, wakati anahangaika kufungua geti, rafiki yake aliyekuwa amelala naye alishtuka na kushangaa kukuta milango iko wazi. Alipotoka nje, akakuta Masogange ndiyo anamalizia kufungua geti kubwa na kuanza kukimbia hivyo akamkimbiza,” kilieleza chanzo chetu.
Akaongeza: “Lakini pia aliwapigia simu marafiki zake wengine na kuwajulisha juu ya tukio hilo, maana mwenyewe ilikuwa mara ya kwanza kumuona katika hali hiyo.”

MASOGANGE ANASEMAJE?
Risasi Mchanganyiko kama ilivyo kawaida yake ya kutokukurupuka, lilimsaka Masogange kwa simu na kufanikiwa ambapo alithibitisha tukio hilo na kufafanua kwamba liliwahi kumtesa kwa muda mrefu huko nyuma, likaisha.

“Ilikuwa hatari sana lakini namshukuru rafiki yangu kwa kunisaidia. Unajua hili tatizo liliwahi kunitesa sana wakati nikiwa mdogo lakini nilikwenda Mbeya nikapewa dawa tatizo likapotea kabisa hadi juzi liliporudi tena,” alisema.
From:GPL