Blogger Widgets

May 24, 2013

Kama Ulikuwa Humjui RAMA MLA NYAMA ZA WATU aliyeachiwa Akiwa na Mama Yake Mahakamani Huyu Hapa

KIJANA Ramadhan Suleiman Mussa ‘Rama mla watu’ na mama yake Khadija Ally, leo wameachiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam  baada ya kubainika kuwa mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo (mla watu) alifanya kosa la mauaji akiwa na matitizo ya akili. Hata hivyo Rama Mla Watu,

ataendelea kukaa katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Isanga mkoani Dodoma mpaka akili yake itakapokuwa sawa ndipo ataachiwa kuwa huru mtaani ili asije akawadhuru watu wengine. Khadija Ally yeye ameachiwa huru. Rama alijizolea umaarufu mkubwa mwaka 2008 baada ya kukamatwa akiwa na kichwa cha mtu kinachodaiwa kuwa ni cha mtoto Salome.  From:GPL