Blogger Widgets

May 14, 2013

Lady Jay Dee Ameanza Kuonesha Kushindwa Kwa Vita ya Clouds Fm Baada ya Kuomba Ushauri wa Kuhamia Kenya au Malawi

165976_10151281153065025_1521636074_n
Malkia wa Bongo Flava maarufu kama Lady JayDee ambae kwa sasa yupo katika ugomvi mkubwa na maboss wa Clouds Media Group ambao ni Bw. Ruge Mutahaba pamoja na Joseph Kusaga.
Sasa imeonekana kama msanii huyu kuanza kushindwa vita alioianzisha dhidi ya hawa watu wawili, ambapo kwa sasa Jide tayari ameshafunguliwa kesi na kutakiwa kurudi tena mahakamani tarehe 25 May mwaka huu. Kwa sasa jide amekatwa na mahaka kuandika au kusema chochote ambacho kinawahusu mabosi hao.
Masaa machache yaliyopita kupitia ukurasa wake wa twitter wa mwanadada huyo nimekuta ameandika @JideJaydee “Kuna muda pesa tu ndio inaongea sijui nihamie Kenya nikaombe uraia huko? Au Malawi labda, mtanifuata?”

Je unafikiri mwanadada Jide ameshindwa kuiendeleza vita alioanzisha??!!