Blogger Widgets

May 17, 2013

Maskini Kangamoja!!! Haoo Mpaka Polisi

JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linalishikilia 
baadhi ya wanenguaji wa kundi maarufu kwa
 kucheza maungo yakiwa wazi ‘Kanga Moko na 
Laki si Pesa’, gazeti la Tanzania Daima la leo l
ina hatimiliki ya hii habari.
Watuhumiwa hao wamekamatwa sambamba
 na watu wengi wanaofanya biashara ya kuuza
 miili yao, kufanya mapenzi hadharani
 na vitendo vya kishoga.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini 
Dar es salaam, Kamanda wa Polisi wa
 Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, 
alisema kuwa kundi hilo sambamba na 
watu hao walikamatwa katika maeneo ya 
Hoteli ya Travertine, Ambiance Club, 
 Kinondoni Makaburini, .“Tumewakamata hao 
wanaofanya mchezo maarufu wa 
Kangamoko na Laki si Pesa na tayari 
 wanafikishwa mahakamani muda wowote 
na msako bado unaendelea ili kudhibiti vitendo
 hivyo na michezo hiyo ya kangamoko au 
baikoko ambayo watu wengi wameilalamikia
 kutokana na mtindo wanaoutumia,” alisema.
Kundi la kangamoko limekuwa likilalamikiwa
mara kwa mara kutokana na kucheza wakionesha
 maungo ya miili yao wazi na kuvaa nguo nyepesi
 wanazozimwagia maji.
Kukamatwa wasanii wa kundi hilo 
kumekuja siku chache tu tangu walalamikiwe 
katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kwamba 
wamekuwa wakipotosha jamnii.
From:AudifaceJackson