MISS Sinza 2011, Husna Maulid, juzikati ameibuka na kudai kwamba katika maisha yake hajawahi kutoa penzi kwa msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Hamis Mwijuma ‘Mwana FA’.
Husna aliyasema hayo Mei 15 mwaka huu baada ya kuvumishiwa kuwa
anatoka kimapenzi na staa huyo na kwamba, kwa sasa hakuna kificho
chochote kwani hadi picha zinazowaonyesha ukaribu wao zimezagaa kwenye
mtandao.
“Sijawahi kutoka na Mwana FA, zaidi ya kufanya naye tangazo
ambalo niliombwa na dada’ngu, Mboni Masimba nikafanye naye kwa ajili ya
shoo ambayo anaiandaa hivi karibuni, wanaonihusisha na mapenzi na Mwana
FA hawanitendei haki hata
kidogo maana sijawahi hata kuwa na wazo naye,”
alisema Husna Maulid.
From:Freebongo
No comments:
Post a Comment