Blogger Widgets

May 24, 2013

Ney wa Mitego Afanya Ngoma Nyingine na Diamond Platnum."After to done did "MUZIKI GANI".....

nay wa mitego


Wimbo uliojizolea umaarufu kwa kipindi kifupi, ‘Muziki Gani’ umeleta neema kwa Nay wa Mitego ambaye hivi sasa ni kati ya wasanii wa bongo ambao ratiba zao zimebanana kutokana na kuwa busy na shows zisizokatika.
Hivi karibuni Nay wa Mitego na Diamond Platnumz wanatarajiwa kufanya tour katika baadhi ya mikoa ya Tanzania ambayo kwa hakika kutokana na ukubwa wa majina yao lazima wataingiza pesa ndefu sana.
Akizungumza na Bongo5 Nay amesema Jumatatu ijayo (May 26) ataachia rasmi video ya ‘Muziki gani’ ambayo itafuatiwa na tour ya kuzunguka mikoani na mpaka sasa mikoa ambayo wameshapata uhakika ni Morogoro, Iringa, Mbeya na Dodoma.
Kutokana na ushirikiano wao wa hit single ya ‘Muziki gani’ kuwa wa mafanikio wameshafanya nyimbo zingine mbili za pamoja ambazo wanategemea kuchagua mmoja kati ya hizo itakayokuwa next single, na pia wana mpango wa kufanya wimbo mwingine wa tatu wa pamoja baada ya kurejea kutoka katika tour ya mikoani.
Hakika hiki ni kipindi cha kumpa tabasamu la muda wote Nay wa Mitego kutokana kuwa na sababu nyingi ikiwemo mpenzi wake anayetarajiwa kumzalia mtoto hivi karibuni, pia show nyingi anazoendelea kuzipata kutokana na single yake ‘Muziki gani’.
Nay hakuwa mchoyo wa fadhila kwa kumshukuru hit maker wa ‘Kesho’ Diamond Platnums kwa kusema amemfanya akaupenda zaidi muziki na kuwa serious nao. “kusema kweli mziki gani imeleta vitu vikubwa imenifanya niufurahie muziki kwa kiasi kikubwa,
imenipa shows nyingi za hela kubwa ambayo nilikuwa sipati katika show za kipindi cha nyuma, na ntakuwa mchoyo wa fadhila nisipomshukuru sana Diamond Platnums ni mshkaji wangu sana lakini amenisaidia mambo mengi sana ambayo huwa tunafanya pamoja” alisema Nay wa Mitego.
Weekend iliyopita Nay na Diamond walijaza watu katika show yao iliyofanyika Dar live, na watatarajia kufanya show nyingine weekend hii pale Maisha club ikiwa ni uzinduzi wa video ya “Muziki Gani”. Huu ndio wakati wako Nay wa kukusanya ku-make money, tunakutakia kila lakheri.