Blogger Widgets

May 22, 2013

Picha ya Ajari Aliyoipata Chris Brown na Mpenzi Wake Karrueche Tran

Mwana R&B Chris Brown mwenye miaka 24 jana Jumanne (May 21) alijikuta katika matatizo baada ya kupata ajali ndogo kwa kuigonga gari nyingine kwa nyuma huko Los Angeles akiwa na ex girl friend wake Karrueche Tran.
Chris ajali-3
Baada ya ajali hiyo Chris alipaki gari yake mbele ya gari aliyoigonga aina ya Mercedes Benz na kusimama pembeni huku dada mwingine wa kizungu (ambaye gari yake imegongwa) akiwa busy na simu. Wakati huo Karrueche Tran alikuwa busy na simu yake ya mkononi akijaribu kufanya u-paparazzi kwa kupiga picha gari waliyoigonga.
chris ajali
Mapema mwezi huu Karrueche alihudhuria moja ya birthday parties za Chris Brown, na Chris hakusita kumpa birthday wishes Karrueche kupitia twitter siku chache zilizopita kitu ambacho kiliashiria bado wana ukaribu.
chris ajali_2

Tukio hili limefungua upya uvumi kuwa huenda Chris Brown na Karrueche Tran wamerudiana japo bado hawajatamka rasmi ikiwa ni siku chache toka Chris aachane na Rihanna.
From:Bongo5