Blogger Widgets

May 18, 2013

Picha ya Mmarekani Aliyecopy Biblia Kwa Kuandika Kwa Mkono wake Kwa Muda wa Miaka Saba wakati Akiwa Muathirika wa HIV

Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Philip Patterson wa New York nchini Marekani ameandika historia kwa ku-copy kwa mkono kitabu cha dini ya kikristo biblia mpaka akakimaliza.
Phillip Patterson
Kwa mujibu wa mtandao wa registerstar Patterson alimalizia kuandika kurasa za mwisho Jumamosi iliyopita, May 11 mishale ya saa 7:20 pm, mbele ya umati wa watu waliofika katika hafla fupi iliyofanyika katika kanisa analoabudu la St. Peter’s Presbyterian huko New York.
Patterson mwenye miaka 63, ametumia miaka 7 kuikamilisha kazi hiyo ya kunakili mamia na maelfu ya maneno yaliyomo katika toleo la zamani na jipya la kitabu hicho cha dini.
Pamoja na Petterson kuwa muathirika wa virusi vya ugonjwa wa ukimwi, alisema hakukata tamaa ya kushindwa kumaliza kucopy biblia wakati bado yupo hai.

Alianza kazi hiyo mwaka 2007, ambayo aliifanyia chumbani kwake katika meza yake ndogo pembeni mwa kitanda, ambapo mwanzoni alikuwa anaandika kwa takribani masaa 14 kila siku na baadae ikawa masaa 8 kwa siku.