Blogger Widgets

May 24, 2013

Picha:Daktari wa Mano Morogoro Kituo Cha Sabasaba Ajinyonga Ndani ya Chumba Cha Kulala Wageni."GEST"

 
MWILI wa Dk Anold Limo ukiwa katika chumba
 cha kuifadhia maiti hospitali ya rufaa ya mkoa wa
 Morogoro muda mfupi kabla ya mwili huo kuondolea
katika nyumba ya kulala wageni ya Camel Nkomola
 Kihonda baada ya uchun
guzi katika hospitali ya mkoa huo mei 22 mwaka huu.
DAKTARI wa meno Anorld Rimo 
(umri wa miaka kati ya 30 hadi 40) wa hospitali ya 
Sabasaba Manispaa ya Morogoro, amekutwa
 amejinyonga katika nyumba ya kulala wageni ya 
Camel iliopo Kihonda.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Faustine Shilogile 
alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei 22 saa 
10 alfajiri katika nyumba hiyo ya kulala wageni.
Alisema Daktari huyo alikuwa amepanga katika 
nyumba hiyo katika chumba namba 2, na kukutwa 
amejinyongea dirishani kwa kutumia foronya za
 mto pamoja na taulo. Ameeleza kuwa usiku wa 
kuamikia siku hiyo marehemu alikwenda katika
 sehemu ya mapokezi ya nyumba hiyo  na kufanya
 fujo na kuonesha sehemu zake za siri kuwa hazifanyi
 kazi.
Kamanda huyo alisema marahemu alikuwa peke yake
 katika chumba hicho na haikufahamika mara moja
 anaishi wapi.

Chanzo cha kujinyonga hakijajulikana na polisi 
wanaendela na uchunguzi.