Blogger Widgets

May 22, 2013

Soma na Sikiliza Point za Mwana FA Juu ya Wasanii wakongwe Kwanini Siku Hizi Hawachoki Kulalamika na Kusema Wanatengwa na Kuleta Matabaka


IMG_0910
Rapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA amesema mara nyingi wasanii wakongwe huishia kulalamika wanapochuja kwakuwa hushindwa kubadilika kuendana na wakati na pia kupenda kuchukuliwa kama ‘malegendary’ hata kama wakichemka kwenye kazi zao mpya.Ameongeza kuwa mara nyingi wasanii wengi hufika hatua ya kuanza kulalamika kwakuwa muziki wa Tanzania hauna mipango inayoeleweka.
“Hivi vitu vingi vinaletwa kwasababu muziki wetu hauna mipango,industry yetu ipo very disorganized. Kwasababu hiyo inafanya watu wamekuwa wakubwa na wamekaa muda mrefu kwenye muziki na nguvu zinaanza kuwapungua wakati hawajafikia yale malengo na wanajiona hawana chochote,”amesema FA.
“Hii inaleta matatizo kidogo. Sitaki kusema vibaya, kiLa mtu ana madai yake pengine na mimi siku moja nitakuja kulalamika, you understand, lakini nachosema ni kwamba nafikiri watu wawe reasonable tuangalie hivi vitu kama biashara, tusiangalie vitu kwa ubinafsi it’s never personal you know,” ameongeza FA.
“Jivishe viatu vya mtu ambaye unamlalamika labda, kama wewe ungekuwa na nafasi yake, na yeye yupo katika nafasi yako ungemtreat vipi nakadhalika. Tusijipe ile superiority complex kwamba mimi ni Mwana FA kwahiyo natakiwa nikitoa wimbo
wangu upigwe kwa hali yoyote, mimi ni AY nikitoa wimbo wangu lazima upigwe kwa hali yoyote ile hata kama nimechemka ama nini.
Tufike mahali tuangalie tushindane na soko kila mtu anafanya muziki wake Mwana FA ni Mwana FA hawezi kushinda na Godzilla hawezi kushindana na Nikki Zohan. Lakini natakiwa nitengeneze class ya Mwana FA niangalie angle ambayo ninatoka, kama siku zote ambavyo tumekuwa tunafanya. Tuangalie kwamba soko limebadilika na inabidi tuende nalo kwa kasi hiyo hiyo badala yake tukitaka kuwa treated kama malegendary tutaishia kulaumu watu tu.”
From:Bongo5

No comments:

Post a Comment