Blogger Widgets

May 20, 2013

Soma Sababu za Spika Wa Bunge Kughaili Kikao Baada ya Mh.Sugu Kuongea Maneno Yafuatayo

waziri kivili wa whvum Joseph Mbilinyi akiwasilisha hptuba ya makadirio-Kambi rasmi ya upinzani
Muda mfupi uliopita spika wa bunge, Anna Makinda amelazimika kusitisha shughuli za bunge mwanzoni tu mwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyokuwa ikisomwa na waziri kivuli wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi aka Sugu.Kauli kwenye hotuba hiyo

iliyobabisha spika wa bunge asitishe shughuli za leo hadi jioni ilisema, “Tanzania imegeuka chini ya usimamizi wa wizara ya serikali hii ya CCM kuwa taifa linalotoka nyara wanahabari, kuwatesa, kuwangoa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua.”

Spika amesitisha bunge hilo ili kupata muda wa kuipitia hotuba hiyo kuondoa kauli za uchochezi.
Sikiliza Alichokisema Hapa Chini

No comments:

Post a Comment