Blogger Widgets

May 22, 2013

Soma Skendo Hii Nyingine Iliyomkuta Msanii Mr. Nice Huko Kenya Mpaka Kuzomewa Club na Kuitwa MACKMUGA


mtandao wa ghafla kutoka Kenya umeripoti kuwa, msanii Mr Nice, amejikuta akizomewa na umati wa watu waliokuwa katika Club moja inayoitwa Iclub, ambapo wachekeshaji Fred Omondi na Mc Antonio hufanya show zao pale kila siku za jumapili.
inasemekana Mr Nice alikua ameenda pale kwa ajili ya kula good time tu, na kufurahisha nafsi yake, lakini matokeo yake hayakua kama alivyotarajia. pale mchekeshaji Mc Antonio alipomuona Mr Nice katikati ya watu, na kwakuwa ni mtu maarufu, Mc akamuambia awapungie mikono watu waliokuwepo pale, lakini Mr Nice hakufanya hivyo wala kusimama akidaikuwa yeye ni msanii ambae amesainiwa na Mc huyo hawezi kumlipa yeye, na akipanda jukwaani hapo atashitakiwa na magement yake.


inasemekana mashabiki walipata kichekesho kipya pale ambapo Mr Nice aliponyanyuka na kusema " Hamnilipi mimi nikipanda hapa kwenye jukwaa, nitashtakiwa mimi" baada ya kusema maneno hayo mashabiki walianza kumzomea huku wakipiga kelele wakisema Mac "Muga" wimbo  wa Ally Kiba, ambao unasemekana kuwa unamdiss yeye. na dj hakuwa na hiyana aliupiga wimbo huo maana mashabiki waliutaka

From:Djfetty