Blogger Widgets

May 30, 2013

Swali Lililokuwa Lisumbua Vichwa Vywa Watu Wengi Kuhusu Marehemu Ngwea Ameacha Mtoto.Sikia Hii Interview


Mwishoni mwa mwaka jana nilifanya interview na marehemu kuhusu maisha yake,historia yake katika muziki na mipango yake katika muziki.Katika interview hii marehemu alizungumza jinsi alivyoingia kwenye muziki,kundi lake la chamber squad,album zake,tuzo na mipango yake kwenye muziki ambapo ilikuwa ni kutoa album ya 3.

Ngwair alisema jina lake halisi ni Albert Kenethj Mangwair, asili yake ni Ruvuma,alizaliwa Mbeya tarehe 16 November mwaka 1983 akiwa ni mtoto wa mwisho kwa baba yake kama mtoto wa 10 na kwa mama yake alisema ni mtoto wa 6.Albert Mangwea alizaliwa Mbeya baadae akahamia Morogoro pamoja na familia, akasoma shule ya msingi Bungo hadi Darasa la 5 kisha akahamia Dodoma pamoja na baba yake nakumaliza shule ya msingi Mlimwa Dodoma.Alivyoenda Sekondari huko ndo alikutana na kina Mez B, Noorah na masela wengine kisha kuanza muziki rasmi nakuweza kurekodi album ya kwanza kama Chamber Squad iliyokuwa inaitwa 'Heshima kwa wote'.

Baadae alikuja Dar  es salaam kisha baadae katika mishemishe za mjini mchizi wake ambaye alikuwa ni msanii pia anayejulikana kwa jina la Tony akaenda nae kwa Majani yaani Bongo Rec ambapo Majani akaona anauwezo nakurekodi ngoma ya kwanza mwaka 2003 kama solo artist iliyokuwa inaitwa 'Geto langu' na ndo ukawa mtoko wa Ngwair.

Marehemua alisema mwaka 2004 ndo alitoa album ya kwanza 'AKA MIMI' iliyokuwa na nyimbo kali kama 'SIkiliza', 'Mikasi' , 'Geto langu' na nyingine kibao na album hii ilimpa tuzo ya Kilimanjaro kama album bora ya Hip Hop,ilifanyika Bongo Rec.Album ya pili ilitoka mwaka 2009 iliitwa NGE ilikuwa na nyimbo kama 'CNN', 'Nipe dili' wimbo ambao ulimpa tuzo nyingine ya Kilimanjaro kama wimbo bora wa Hip Hop.

Katika interview hiyo Marehemu alimtaja msanii wa Tanzania aliyekuwa akimsikiliza na alikuwa akimpenda kabla hajatoka na hata baada ya kutoka ni Profesa Jay.Pia.Katika interview hiyo Ngwair alisema kuwa ana mtoto mmoja.

*Marehemu Ngwair alisema kuwa hajawahi kuwa na bifu na msanii yeyote.
*Alipenda kujiita aka Cowboy kutokana nakupenda maisha ya Shamba.
* Marehemu alisema alisomea Ufundi katika chuo cha ufundi Mazengo,ufundi mwashi
*Alisema kuwa ana mtoto mmoja

SIKILIZA interview hiyo hapo chini From Anna Peter

No comments:

Post a Comment