Blogger Widgets

May 18, 2013

Uvumi umetokea Kwamba Kanye West Ni Shoga,Check Baadhi ya Picha Mbalimbali Akiwa na Huyu Mtu Kutoka Paris

 
Jarida la In Touch limeandika, muigizaji nyota ambaye kwa sasa ni mjamzito Kim Kardashian, anahofia boyfriend wake Kanye West huenda akawa ni shoga na ana boyfriend jijini Paris.

Kwa mujibu wa jarida hilo, Kardashian anapata wasi huo sababu watangazaji wengi wa kwenye mitandao wanamuhisi kwamba boyfriend wake huenda akawa yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume ambaye aliwahi kumtengenezea nguo aitwaye Riccardo Tisci.”

Japo yeye anamuita "rafiki" alilieleza kwenye jarida hilo, “Kim alifunguka zaidi na kusema. Kama kweli ikitokea kwamba Kanye yupo na Riccardo kimapenzi, itamumiza sana - zaidi ya nilivyowahi kuumizwa kwenye maisha yake yote.”
Jarida la In Touch limeandika, “Kuna vielelezo ambavyo Kim hawezi kuvipinga,” huku vikiorodheshwa, “Katika kipindi chote ambacho Kim ni mjamzito Kanye amekuwa akitumia muda wake mwingi akiwa karibu na Riccardo kwenye jiji hilo lililopo nchini Ufaransa… Na hivi karibuni Riccardo amenunua nyumba New York umbali wa nusu ya maili toka sehemu ambayo Kanye anaishi.”

kanye-west-Riccardo-Tisci

Swali linakuja kwamba pamoja na hayo yanayozungumzwa iwe ni ya kweli au ni uzushi lakini Kim K ambaye amebeba kiumbe cha Kanye anajisikiaje na analichukuliaje swala hilo?
Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Radar online kuwa Kim hajaamini maneno yanayozungumzwa mtaani kuwa mpenzi wake ni shoga na anachukulia uvumi huo kuwa ni wa kushangaza. Chanzo kimeendelea kusema uvumi huo unamkasirisha sana mama kijacho sababu unawaletea usumbufu mkubwa kutoka kwa waandishi wa habari, na pia mtu yeyote anapomzungumzia vibaya Kanye inamkosesha sana raha na kumwongezea hasira.
Hivi karibuni Kanye west amezushiwa kuwa na mahusiano na mwanaume aitwaye Riccardo Tisci ambaye wamekuwa wakionekana pamoja mara kadhaa.