Blogger Widgets

June 1, 2013

Angalia Kauli ya Soggy Soggy Kuhusu Unafki Unafanyika Kwenye Huu Msiba wa Marehemu Albert Mangwea

Kipindi hiki cha msiba wa the most talented rapper, freestyler mwanachemba Albert Mangweha, wasanii wa muziki wa kizazi kipya, maproducer, watangazaji wa radio na TV pamoja na wadau wengine wameonesha umoja na mshikamano kwa kuungana na kusaidia familia ya marehemu kwa kuchangia gharama za shughuli mbalimbali za msiba huu.
soggy-3
Tunajua kuchanga ni jambo la hiari kwa kila mmoja kulingana na moyo unavyomtuma mtu, lakini pia hali halisi ya maisha ya kila mtanzania, kitu ambacho kinasababisha wawepo watu wanaoweza kuonyesha mapenzi yao kwa mchango wa pesa na wengine kuonyesha tu hisia zao na nia hata kama hawana uwezo wa kuchangia chochote.
Rapper Soggy Doggy a.k.a Chief Rumanyika yeye amejaribu kuwakosoa mashabiki ambao huwa wanajaa katika show za wasanii lakini wanashindwa kumchangia gharama za msiba pale msanii anapoaga dunia.

Soggy alitweet, “#MSANII ana uwezo wa kukusanya watu 7,000 kwenye show na wote wamelipa halafu akifa mnagoma kuchanga hata 1,000 kwa M-pesa!Huo ni USNITCH”.
Watu wote walioguswa na msiba huu wanahamasishwa kuendelea kutoa michango yao kwa kupitia namba za akaunti ya benki, na simu zilizotolewa na kamati, pia kwa walioko Dar wanaweza kuwasilisha michango yao pale Leaders Club kwa kamati, au nyumbani kwa kaka wa Mangweha ulipo msiba Mbezi beach, Goigi.