Blogger Widgets

June 1, 2013

Baadhi ya Picha Mbalimbali za Maandalizi ya Mazishi Huku Morogoro

 Msemaji wa familia hiyo Bw Daniel Mangwea ambaye ni baba mdogo wa marehmu Albert akizungumza na Mwandishi wa audifacejackson leo asubuhi.Familia ya marehemu Albert Mangwea imedai kwamba kwa sasa wana upungufu wa viti na maturubai hivyo mtu yoyote mwenye vitu hivyo anaombwa kuvipeleka nyumbani kwa mama mzazi wa msanii huyo Kihonda Mazimbu Road.Akizungumza na  Mwandishi wa audifacejackson blog leo leo asubuhi msemaji wa familia hiyo Bw Daniel Mangwea alidai kwamba tatizo walilonalo kwa sasa ni upunguvu wa viti na maturubai.
 Baadhi ya waombolezaji wakimfariji mama mzazi wa Albert Mangwea Bi Denisia Mangwea.

 Padre wa kanisa katoriki Parokia ya Mtakatifu Monica Kihonda Fr Octavian Msimbe ambaye ndiyer anayetarajiwa kuongoza misa ya mwisho ya marehemu Albert Mangwea.
 Pilika pilika za maandalizi ya kupokea mwili wa Albert Mangwea zikiendelea kwa sasa nyumbani kwao Kihonda Mazimbu Road
HAPA ndipo nyumbani kwa marehemu mzee Keneth Mangwea Kihonda Mazimbu Road mkoani Morogoro ambako mwili wa Albetn Mangwea  utapunzishwa hapa kabla ya kwenda kuzikwa 
From:Audifacejackson