Blogger Widgets

June 29, 2013

Baby Madaha alia na Kufuri zake(Nguo za Ndani)

KATIKA hali ya kushangaza, msanii wa filamu na muziki Baby Joseph Madaha amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuibiwa nguo zake za ndani alizokuwa ameanika nje maeneo ya Mikocheni jijini Dar.
Chanzo  cha habari ambacho ni shosti wa karibu wa mwanadada huyo kilichoomba hifadhi ya jina lake kilitiririka:
“Alizifua kama dazeni nzima hivi na kuzianika nje kisha kwenda kwenye mishe zake. Heh! Kumbe vibaka hawaachi kitu, waliruka fensi wakazichukua pamoja na ndala.”
Katika kujua ukweli wa habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Baby Madaha na alipopatikana alisema ni kweli alilizwa nguo hizo na kudai anafanya jitihada za kuhama kwani eneo analoishi limezidi kwa wizi.