Blogger Widgets

June 2, 2013

Check Picha za Mshiriki wa Kenya X-Girlfriend wa Prezoo,The Lady Boss Huddah Akimwaga Machozi Wakati Akielezea Jinsi Alivyomiss Mapenzi ya Kitandani ya Boyfriend Wake

Shindano la Big Brother Africa 2013 lilopewa jina la “The Chase” linaendelea huko Afrika Kusini na katika siku ya sita mrembo kutoka Kenya Huddah Monroe amedodosha machozi huku akisimulia wazi zile moment za mahaba ya ndani alizomiss kwa chalii wa Kenya. 

Huddah alifunguka wakati alipokuwa na maongezi ya ndaani na mshiriki  toka Afrika Kusini Angelo wakishare masimulizi ya mapenzi na jinsi wanavyowamiss wapenzi wao kwa kuwa ndani ya mjengo huo.

The Kenyan boss Lady alisema, “ I miss the way he kisses me, I miss him biting my neck.” Ni moja kati ya vitu alivyovikumbuka Monroe. Angelo alimuuliza kama anauhakika na mahusiano yao na anauhakika na huyo jamaa, alijubu kwa ufupi tu kuwa anamuelewa, “he understands me.”

Hakutaja jina la mpenzi wake huyo aliyemtoa machozi baada ya kumkumbuka wakiwa faragha.

Huddah na Prezzo walikuwa wapenzi na hadi sasa inaonesha bado wana mahusiano flani japo hakuna uhakika kama ni ya kimapenzi. Hivi karibuni Prezzo amejiung na kampeni ya kumpigia debe Huddah ili apate kura za kumbakiza kwenye mjengo huo.

Leo (jumapili) ni siku ambayo washiriki kadhaa watafungasha mabegi yao na kurudi kwao na wengine kuokolewa na kura za watazamani, Huddah ni mmoja kati yao. Wengine ni Betty, Denzel, Natasha na Selly.
 
From:Leotainment