Blogger Widgets

June 16, 2013

Hali Ilivyo Mida Hii Ndani ya Jiji la Arusha Baada ya Tukio la Jana La Kujeruhiwa Watu

          


HIVI SASA UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA HUKU ENEO LA TUKIO LIKIWA LIMEZIBWA NA TURUBALI UCHUNGUZI UKIENDELEA KUFANYWA. ENEO HILO BADO LIMEJAA WATU AMBAO HAWAAMINI KILICHOTOKEA JANA NA KUENDELEA KULALAMA. HABARI ZAIDI ZITAKUJIA.
Photo Credits: ALBERT BALATIJana Ilivyokuwa

Jaji mstaafu wa Mahakama ya rufaa Damian Lubuva ambae ni mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema “Jioni ya June 15 2013 tulipata taarifa ya tukio kule Arusha ambako uchaguzi unafanyika katika kata nne za pale mjini, katika kata moja wapo ya kumalizia kampeni za mwisho bomu likatupwa na watu kufariki pamoja na wengine kuumia, kutokana na hilo tumeona sio wakati muafaka kwa uchaguzi kuendelea kwa sababu wengine wanaendelea na shughuli za mazishi” “Tume imeahirisha uchaguzi katika kata nne za Arusha mjini kutokana na tukio hilo ambalo linawapa Wananchi hofu wakati wa kupiga kura hivyo uchaguzi umeahirishwa hadi tarehe 30 June” – Lubuva


Majeruhi. Mungu urehemu tz