Blogger Widgets

June 3, 2013

Hatimaye Show ya Lady Jay Dee na Mwana FA Kugongana Tena Siku Moja


Ikiwa ni siku chache baada ya wasanii kuahirisha show zao kufuatia kuondokewa mpendwa wetu Albert Mangwea, miongoni mwa show kubwa zilizoahirishwa ni ya Lady Jay Dee (Miaka 13 ya Lady JayDee) na ya Mwana FA (The Finest) zilizokuwa zifanyike siku moja (May 31),show hizi zinaweza kufanyika tena siku moja kwa kuwa wasanii hao wametaja tarehe inayofanana.

May 28 ambayo ndiyo siku aliyofariki Mangwea mwana FA alithibitisha kuahirisha show yake, lakini alipoulizwa siku ambayo anadhani atairudia show hiyo, yeye alifunguka kupitia akaunti yake ya twitter na kuitaja June 14.

 “Sina uhakika,but I'll pick June 14th kama brother tutakuwa tushampumzisha"@umykitwana”, alitweet Mwana FA a.k.a Binamu.
Kwa upande wake Lady Jay Dee ambae kwa sasa a.k.a yake mpya ‘Anaconda’ inaonekana ku-take over ametumia akaunti yake ya twitter kuiweka wazi tarehe ya show yake alipokua akijibu swali la fan wake ambae atasherehekea siku moja ya kuzaliwa na msanii huyo (June 15).

“@MteiHaikaJ Gud. Chukua hii tar 13 June Mahakamani, tar 14 June miaka 13 ya Jide na tar 15 June Bday ya Jide. Let's celebrate long week end.”Alitweet Lady Jay Dee June 2.

Kwa tweets za wakali hawa wa bongo fleva inaonesha kabisa kuwa show zao zinaweza kufanyika june 14 japo Mwana FA alisema hana uhakika, labda kama atatangaza siku nyingine tena. June 14,tunatarajia kuwa marehemu Ngwair atakuwa amekwisha pumzishwa kwenye nyumba yake ya milele huko Morogoro.

No comments:

Post a Comment