Blogger Widgets

June 7, 2013

Huddah wa Kenya apokelewa na Prezzo akitokea Afrika Kusini Juzi, akutana na waandishi wa habari (picha) angalia hapa wakiwa pamoja na Prezoo

 Jana jioni mrembo Huddah Manroe aliwasili nchini Kenya mida ya jioni akitokea nchini Afrika Kusini na kama ulikuwa hufahamu alipokewa katika uwanja wa ndege na rapper CMB Prezzo!, nahisi ume ‘wow’ right?

Inavyoonekana kile alichokuwa anakizungumza Huddah mjengoni kuhusiana na Prezzo sasa ameamua kukitolea uthibitisho kuwa ni wapenzi (kwa mujibu wa maelezo ya Huddah na mapokezi hayo) na kuamua kuwafunga midomo ‘haters’ kwa kupiga picha za pamoja wakitokea uwanja wa ndege .

Baada ya kuwasili uwanja wa ndege Huddah na Prezzo walipanda gari moja na kuelekea walikoelekea!, na kupiga picha zinazoonyesha uhai wa mahaba, kama unajua kusoma ‘body expressions’ ambazo kama Huddah angekuwa mpenzi wa mipasho huenda angeziwekea caption ya “wenye wivu wajinyonge’!.

Ikiwa ni siku yake ya kwanza toka awasili Kenya staa huyo Huddah leo alikuwa na mkutano na waandishi wa habari kwaajili ya kuzungumzia ushiriki wake katika Big Brother ‘The Chase’ na kujibu maswali ya waandishi.
Siku ya leo Huddah ameonekana kuwa dhabahu inayosakwa na watu wengi ambao kila mmoja anataka kuonana nae.