Blogger Widgets

June 16, 2013

List ya Washindi wa Tuzo za Steps Bongo Movie Awards


Kampuni ya usambazaji wa filamu Tanzania ya Steps Entertainment Limited, jana imettoa tuzo kwa wasanii, Watayarishaji, Waongozaji na wadau mbalimbali waliopo katika tasnia ya filamu Tanzania. Shughuli ya utoaji wa tuzo hizo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza kuanzia saa 1:00 usiku.
Meneja Masoko wa Steps Entertainment, Kambarage Ignnatus akionyesha moja ya tuzo zitakazotolewa kwa wasanii leo kwenye ukumbi wa Blue Pearl.
Meneja Masoko wa Steps Entertainment, Kambarage Ignnatus akionyesha moja ya tuzo zilizotolewa kwa wasanii leo kwenye ukumbi wa Blue Pearl.

Tuzo ambazo zilitolewa usiku wa jana zikihusisha zaidi wasanii wanaofanya kazi na kampuni yao tu. Tuzo ambazo zimetolewa ni pamoja na filamu bora ya mwaka, Kampuni iliyotengeneza filamu bora, msanii anayependwa na watu ndani na nje ya nchi, msanii bora chipukizi, mwigizaji bora wa kike, mwigizaji bora wa kiume, mwongozaji bora wa filamu na mwandishi bora wa filamu.
Mratibu wa tuzo hizo, Carlos Johns Silondwa amesema wameandaa tuzo hizo kwa lengo la kuleta ushindani na kukubali mchango wa wasanii, watayarishaji na wadau wote na pia ni kuwatambua na kujali mchango wa wasanii katika ukuzaji wa filamu nchini, ambapo tuzo hizo ni kichocheo kitakacholeta ushindani unaoweza kujenga tasnia ya filamu na kujenga ajira kwa jamii kubwa.
“Tunaamini kuwa tuzo zitakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza tasnia ya filamu, kuongeza ushindani katika kutengeneza filamu bora, hadithi nzuri zinazoelimisha, kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania,” alisema Silondwa.
.
Tuzo zimetolewa June 15 2013
Mwigizaji bora wa kiume 2012 ni JB ambae ameng’aa kwenye movie ya ‘Nakwenda kwa mwanangu’ aliyocheza na mzee Majuto. Mwigizaji bora wa kike 2012 ni Irene Uwoya. Best movie 2012 ni Kijiji cha Tambua haki ya marehemu Kanumba Movie iliyouza sana 2012 ni Ndoa yangu ya Steven Kanumba. Best Action movie ni ya Jimmy Master ya Double J Best Negative role ameshinda Chek budi Mwigizaji bora chipukizi ni Niva. Best Supporting Actress ni Riyama Ally Mwigizaji bora chipukizi wa kike ni Irene Paul. Mchekeshaji bora 2012 ni King Majuto……

Mwongozaji bora wa filamu 2012 ni Vicent Kigosi (Ray)