Blogger Widgets

June 7, 2013

M2 The P Alonga Machache Kuhusu Kilichotokea Kwa Mujibu wa NIPASHE

Msanii 'M 2 the P' ambaye alikuwa na marehemu Albert Mangweha nchini Afrika Kusini wakati rapa huyo anafariki na yeye pia kuzidiwa hadi kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, alihudhuria mazishi mjini Morogoro jana.

'M 2 the P' ambaye awali naye aliripotiwa kuwa amefariki kabla ya taarifa hizo kukanushwa, alisema jana kuwa hadi sasa hajui nini kiliwatokea.

Msanii huyo alisema kwamba hakumbuki kilichotokea hadi wakazidiwa na kukimbizwa hospitali wakiwa hawajitambui.

Alisema pia bado anajisikia anaumwa hadi sasa licha ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya St. Hellen Joseph ya Afrika Kusini alikokuwa amelazwa.
chanzo:nipashe