Blogger Widgets

June 10, 2013

Matukio Kumi ya Kuchekesha,Kusikitisha na Kufurahisha Umati kwenye Tuzo za Kil Music Awards

Ingia ndani kusoma Matukio 10 ya kukumbukwa/yaliyoshangiliwa zaidi kwenye tuzo za Kilimanjaro mwaka 2013.
Shilole kulia kwa furaha baada ya Kala Jeremiah kushinda tuzo
IMG_4286
Kila mmoja kwenye ukumbi alikuwa na shauku ya kumjua msichana aliyemkimbilia na kumkumbatia huku akilia kwa machozi mengi Kala Jeremiah baada kutajwa mshindi kwenye tuzo ya kwanza.
IMG_4290
Msichana huyo alikuwa Shilole. Wengi walihisi huenda Shilole na Kala ni wapenzi lakini leo June 10 tumeongea na wote kwa pamoja na kusema wamefahamiana muda mrefu sana, kiasi cha kuwa kama mtu na kaka yake wa damu. Shilole alisema anafahamu Kala alivyosota na hivyo kitendo cha kuona ameshinda tuzo kilimfanya ashindwe kuyazuia na kulia kwa furaha.
Hussein Jumbe kucheza kama TID wakati akiperform Zeze
IMG_42131
Katika kitu ambacho KTMA mwaka huu imefanikiwa ni jinsi walivyopanga wasanii wapya waimbe nyimbo za wakongwe na wakongwe waimbe nyimbo za vijana wao. Aliyetia fora zaidi ni Hussein Jumbe aliyeimba kwa mbwembwe wimbo wa TID, Zeze na kujitahidi kucheza kama vijana. Mzee alipata shangwe za kutosha.
King Crazy GK kupanda jukwaani kutaja wimbo bora wa Hip Hop
IMG_4293
Ilikuwa ni surprise ya aina yake kumuona GK kwenye stage. Watu wengi walisikika wakisema wamemmiss na kumtaka aimbe kidogo. Jamaa alishangiliwa sana na hiyo ni ishara kuwa muziki bado unamhitaji.
Barnaba kumrukia Amini baada ya kushinda wimbo bora wa Zouk/Rhumba
IMG_4230

Baada ya Amini kutajwa mshindi kwenye kipengele cha wimbo bora wa Zouk/Rhumba wana THT wote walikimbia kwenye stage kumpongeza Amini. Lakini Barnaba aliamua kwenda mbali zaidi kutokana na furaha yake baada ya kumrukia Amini aliyempakata kama baba aliyempaka mwanae aliyemmiss kwa muda mrefu ama kama vile mke anavyomrukia mume wake amwonapo kwa mara ya kwanza baada ya kuachana kwa muda mrefu. Ilikuwa raha sana.
Afande Sele kuanza kuleta maneno mengi kiasi cha Dj kumkata ili aanze kuimba IMG_43761
Kama kawaida Afande Sele alipanda stage na mizuka ile ile ya kush!! Dj alimwekea beat yake ili aanze kufanya yake lakini alimzuia DJ kwanza na kuanza kutoa nasaha kadhaa na siasa kibao na hivyo kuchukua muda kuliko aliopangiwa na kumfanya DJ amuingilie kati kumshtua‘time is money bro, quit the blah blah blah and sing!!
Story na vituko vya Zembwela IMG_3225
Zembwela alifunika sana kutokana na story zake za kuchekesha. Kila zamu yake ilipofika watu waliandaa kabisa mbavu zao kucheka. Standup comedy anaiweza sana huyu jamaa.
Gadner alipopanda jukwaani kuchukua tuzo ya Lady Jaydee

IMG_4365
Gadner alipanda kwenye stage kuchukua tuzo ya mkewe, Lady Jaydee na kusindikizwa na masela kibao. Wakati anaongea kulikuwa kukisikika sauti nyingi zikimtaka aitaje tarehe ya show yake ya June 14. Watu walishangilia sana.
Member wa Jambo Squad kuilamba trophy
IMG_3253
Mamong’oo wa Arusha walitisha sana kwa jinsi walivyokuwa wakiongea. Mmoja wa member wa kundi hilo aliamua kuilamba trophy ili kuonesha furaha aliyokuwa nayo. Shangwe lake lilikuwa aibu!!
Performance ya Barnaba

IMG_4301
Barnaba akiwa na guitar lake alionesha ukomavu kwenye stage. Aliimba wimbo wake Sorry uliofanya usikike kama wimbo uliopigwa na band ya Uingereza ya Coldplay. He killed it.
Performance ya Jose Mara
IMG_4346
Jose Mara ndiye msanii aliyetuzwa fedha nyingi zaidi hasa na wanawake. Aliimba wimbo maarufu wa Njenje, Kinyaunyau na ukumbi wote ulikuwa ukumuitikia ‘HALOOOOOOOOOOO’ kila alipoimba ‘mimi nina wangu nyumbaniiiiiiiiii’
From:Bongo5