Blogger Widgets

June 4, 2013

P Funk Majani Achanganikiwa Baada ya Kuliona Jeneza La Marehemu Albert Mangwea na Kuanza Kubujika Machozi Huku Akilisukuma Gari

P Funk Majani akisisitiza jamboEditruda Mashimi,Dar es Salaam
MWANDAAJI wa ala za muziki nchini Tanzania  P Funk Majani alichanganyikiwa baada ya kuona jeneza iliyokuwa imebeba mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea.
P Funk ambaye muda wote alikuwa amekaa kwenye gari akiwa na huzuni mkubwa kufuatia kifo cha msanii huyo, alibadilika ghafla baada ya kuona jeneza hilo likiingizwa katika gari maalum tayari kwa ajili ya safari kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
P Funk alishindwa kujizuia na akalazimika kushuka kwenye gari lake na kwenda kusukuma gari lililokuwa limebeba mwili wa msanii huyo aliyefariki Dunia Mei 28 mwaka nchini Afrika Kusini.
Kitendo cha P Funk kusuka gari hilo huku akibubujika machozi kwa zaidi ya dakika mbili ilihamasisha mashabiki wa msanii huyo na kuungana naye kusukuma gari hilo.
Tukio hilo lilitokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakazi wa jiji la Dar es Salaam kesho watapata fulsa ya kutoa heshma ya mwisho kwenye jeneza la marehemu Mangwea katika Viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Mjini Morogoro kwa mazishi kesho kutwa.