Blogger Widgets

June 15, 2013

Picha Ikionesha Jinsi Jacklyn Wolper na Monalisa Walikutwa na Mr.Camera Man wakishindana Kukata Viuno kwenye PartyBURUDANI ya aina yake imetokea baada ya mastaa wenye heshima kubwa kwenye soko la filamu Bongo, Jacqueline Wolper na Yvonne Cherry ‘Monalisa’ kunaswa wakishindana kukata mauno.


Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kwenye send off ya mwigizaji mwenzao, Flora Mvungi iliyofanyika Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Msasani Beach, Mikocheni jijini Dar ambapo ulipofika wakati wa kuserebuka, mpambano huo wa kukatika ulianza.


Awali walianza kwa staili ya taratibu, baadaye muziki ulipochanganya walianza ‘kuchimba’ staili ya kiduku hadi chini huku wakionesha utundu wa hali ya juu wa kukata nyonga.

“Mh! Leo lazima tumpate mshindi wa kweli, Wolper anayaweza lakini hata Mona naye yupo fiti daah! Burudani kweli leo hahaha!,” alisikika mgeni mwalikwa aliyejitambulisha kwa jina moja la Salma na mpaka mwisho, waalikwa wengi walihitimisha kwa kusema hakuna mshindi.