Blogger Widgets

June 3, 2013

Picha Jinsi Albert Mangwea Alivyoagwa Huko South Africa Wakishirikiana na Bushoke




Wadau wa Afrika Kusini wakiwa katika harakati za kuusafirisha mwili wa msanii wa kizazi kipya aliyefariki Dunia huko nchini Afrika ya Kusini hivi karibuni,marehemu  Albert  Mangwear jioni hii huko  Johannesburg, Afrika Kusini. Ratiba zinaonesha mwili huo utawasili kesho jijini Dar es salaam. Muda na ratiba kamili zitafuata punde



Watanzania waishio nchini South Africa wamepata nafasi ya kuuaga mwili wa Albert Ngwea kuelekea katika safari ya mwisho wakiongozwa na Msanii Bushoke na Mtoto wa Mhe. Kingunge Ngombale mwiru, Kinjeketile wanaosimamia mipango ya kuaga mwili nchini Afrika kusini...



Mwili  wa  marehemu  utaletwa Tanzania  kesho  saa  nane.....


 


Watanzania waishio nchini South Africa, wamepata nafasi ya kuuaga mwili wa mwanamuziki ALBERT MANGWEA aliefia nchini humo … Hii hapa chini moja ya picha inayoonesha watu wakiaga mwili huo …
Ngwair-SA
Mwili wa Marehemu Ngwair utawasili kesho jijini Dar Es Salaam na kuagwa na fans, marafiki na ndugu katika viwanja vya leaders club, kinondoni kabla ya safari ya kwenda Morogoro, ambapo atazikwa huko karibu kabisa na kaburi la baba yake mzazi …
R.I.P Albert Mangweha.

No comments:

Post a Comment