Raia walipoamua kufunga barabara na kuchoma moto
HABARI KAMILI JUU YA KILICHOSABABISHA: Jeshi
la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na
maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu
kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea
kwenye viwanja hivyo .
Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema
kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo
imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu
upelelezi.
Kamanda
Sabas amedai kuwa jeshi la polisi liliwataka viongozi wa chama hicho
kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo
lakini si kwenye viwanja hivyo.
Hali
kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa
chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza
..
Hata
hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo hilo
na kuanza kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA , hali iliyoleta mvutano kati ya viongozi wa jeshi la polisi na wafuasi hao.
Wakati mabishano hayo yakiendelea,
Askari Polisi mmoja alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa
Chadema pembeni mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu
wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa na bomu June 15 2013.
Baada ya hapo,Wafuasi hao hawakupenda
kitendo cha Polisi kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka
atoke, baada ya dakika kadhaa mabumu yalianza kusikika.
Baadhi
ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani haponi mbunge wa
jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje,Tundu lissu, Halima Mdee... |
No comments:
Post a Comment