Blogger Widgets

June 16, 2013

Soma Kituko Alichoonesha Kanye West Baada ya Mpenzi wake Kim Kardashian Kujifungua Mtoto wa Kike JanaIkiwa ni wiki moja tu toka Kanye Omari West (36) ‘Kanye West’ asheherekee birthday yake (June 8), mpenzi wake Kimberly Noel “Kim” Kardashian (32) jana Jumamosi (June 15) amejifungua mtoto wa kike ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya muda uliotegemewa.
Kim giving birth
Vyanzo vilivyo karibu na KK vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Kim alijifungua salama kwa njia ya kawaida (Natural child birth) na huku akiwa amewahi kwa wiki 5 kabla ya tarehe iliyokuwa inategemewa.
Vyanzo hivyo vinasema Kim alianza kupata dalili Ijumaa usiku (June 14) na siku iliyofuatia Jumamosi asubuhi alipelekwa katika hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center huko Beverly Hills,na kupelekwa moja kwa moja sehemu ya kujifungulia, na akajifungua jana Jumamosi (June 15).
Cedar hosp Hili ndio jengo la hospitali ya Cedars-Sinai alipojifungulia Kim K
Cedars-Sinai ni hospitali ambayo mastaa wengi wamejifungulia watoto wao akiwemo Britney Spears, Jessica Simpson, Victoria Beckham na wengine.
Baba wa mtoto Kanye West hakuwa mbali na mpenzi wake toka wanafika hospitali mpaka katika chumba cha kujifungulia alikuwepo pembeni ya KK huku akishuhudia zoezi zima hatimaye mwanao akaanza kuvuta hewa ya duniani.

Vyanzo hivyo vimeendelea kusema Kanye West alilazimika kutohudhuria listening party ya album yake mpya (Yeezus) iliyofanyika Ijumaa usiku (June 14), mara tu baada ya Kim kumwambia hajisikii vizuri ilimbidi arejee nyumbani na Jumamosi asubuhi akaongozana na mpenzi wake mpaka hospitali.
Kim K na mwanae ambaye bado hatujajua atapewa jina gani wako na afya njema, vyanzo vimethibitisha.
Huyu ndie mtoto wa kwanza wa mastaa Kanye West na Kim Kardashian.
"Simamisha muziki na wote mpige kelele kwa mama kijacho," alisema West jukwaani akionyesha kidole kwa Kim ambaye alikuwa mmoja wa  watazamaji.