Blogger Widgets

June 18, 2013

Take This:Video ya Ikionesha Jinsi Yule Dada wa Kitanzania aliyekatwa na Madawa ya Kulevya Misri Akiwa Anahojiwa Kwa Mara ya Kwanza

Kwa zaidi ya wiki moja iliyopita habari zilisambaa kwamba binti Mtanzania aliekamatwa na dawa za kulevya nchini Misri angenyongwa siku za karibuni kutokana na hizo dawa alizokamatwa nazo.
millardayo.com baadae ilimpata balozi wa Tanzania Egypt ambae alikanusha taarifa za kunyongwa na akakubali kwamba kweli kuna Watanzania wawili wamekamatwa ambao ni huyo msichana na ndugu yake wa kiume ambao ni wakazi wa Magomeni Dar es salaam na kwamba wanashikiliwa na polisi huku wakisubiri kesi yao.
Check video ya mahojiano ya TV na msichana huyu ambae anadai alikwenda Misri kumtafuta binamu yake, begi alilokamatwa nalo ni lake ila alikua hajui kama lina dawa za kulevya.