Blogger Widgets

July 29, 2013

Angalia Picha za Jinsi Msanii wa Kike wa Bongo Alivyotembelea Kabuli la Mangwea

Dayna akiweka Mshumaa juu ya Kabuli 
     Mwimbaji wa nyimbo  za mafungu ya nyanya, Fimbo ya mapenzi, Nivute kwako na ule unaotamba sasa wa Leo, Dayna Nyange  mkali wao,  ndani ya mwezi mtukufu, amefanya ziara ya kumkumbumbuka na kutembelea kaburi alilozikwa mwanamuziki mwenzie toka Morogoro, Albert Mangwea
     Dayna ameonekana katika kabuli la Mangwea, mwanzoni mwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Akizungumza na mwandishi wa Habari hii mara baada ya tukio, Dayna amesema Albert Mangwea  ni mmoja  ya wasanii aliokuwa nao karibu sana na alikuwa  akimsaidia kwa mambo mengi sna katika mziki
   "Unajua Albert Mangwea ni zaidi ya msanii mwenzangu, alikuwa kama ndugu kwangu. Albart alikuwa akinishauli mambo mengi sana juu ya mzikim na hata maisha pia. Hivyo ni wajibu kwangu kumkumbuka mara kwa mara.  Pia kitu ambacho hukijui, Ngwea ni mmoja ya wasanii walionisaidia sana hasa kusambaza wimbo wangu huu wa sasa nilioimba na Mr: Blue - Leo. sitamsahau my Brother Ngwea  na ndiyo maana ndani ya mwezi mtukufu nimetenga siku ya leo kuja kumtembelea. Pumzika kwa amani japo pengo lako bado lipo'' Amemaliza huku akibubujikwa na machozi.
Dayna akipiga saluti ishara ya kumkubali Marehemu Albert Mangwea
Pumzika kwa amani Ngwae.