Blogger Widgets

July 24, 2013

Aunt Ezekiel Aingia Kwenye Kashfa Nyingine ya Ngono.SOMA HII

Aunt Ezekiel akiwa amepoozi na pozi tulivu.


MWIGIZAJI wa filamu Aunt Ezekieli amekaliwa kooni na Serikali kupitia bodi ya filamu iliyomtaka aondoe baadhi ya vipande vinavyohamasisha ngono, katika sinema yake mpya iitwayo Scola.
Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo inayosimamia maadili ya sinema za Kitanzania, imeeleza kuwa Aunt aliipeleka filamu hiyo ili ikaguliwe kama zilivyo taratibu, lakini bahati mbaya ikabainika kuwa kuna ‘sini’ tatu ambazo zilitoka nje ya maadili ya mtanzania.
“Katika sinema hiyo kuna sehemu kama tatu ambazo kimsingi zimevunja maadili ya kitanzania hivyo ni lazima avitoe kama anataka kuingiza sokoni sinema hiyo”,ilisema shemu ya taarifa hiyo.
Akizungumza na Habarimpya.com rafiki wa karibu wa Aunt Ezekieli alisema kuwa rafiki yake (Aunt) amekaliwa kooni na bodi hiyo, lakini bado yupo katika mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa aendelee na maandalizi ya mwisho ya filamu kabla ya kuingia sokoni".
“Amejaribu kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie mtaani pasipo kuviondoa hivyo vipande, kwa madai kwamba navyo vina umuhimu wake lakini amekataliwa" alisema rafiki wa Aunt kwa sharti la kutotajwa jina mtandaoni.
Hata hivyo jitihada za Habarimpya.com kumtafuta Aunt ili kujua undani wa suala hilo ziligonga mwamba, baada ya siku yake ya mkononi kuita bila kupokelewa kwa zaidi ya saa tatu.

Mwaka jana mwishoni, bodi ya filamu ilimzuia mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ kuingiza sokoni sinema ya Sister Mary baada kutoridhishwa na uandaaji mwake uliokuwa umechukuwa asilimia kubwa ya kulidhalilisha kanisa katoliki katika sinema hiyo.

From:Habari Mpya