Blogger Widgets

July 18, 2013

Check Picha Jinsi House Girl Alivyokutwa Akiuza Kwenye Duka La Madawa Baada ya Kuwa Kero kwa Wateja wa Duka Hilo Kupewa Dozi Ndivyo Sivyo

Baada ya OFM kupokea taarifa hizo, ilianza utafiti wake ambapo iligundua kuwa mmiliki wa duka hilo anatambulika kwa jina la mama Atu.
Ikadaiwa kuwa mmiliki huyo ana tabia ya kumuachia duka hilo hausigeli wake aitwaye Furaha ili auze dawa kwa kubahatisha na mara kadhaa wagonjwa hupewa dozi ndivyo sivyo.
“Kuna mwenzetu alikuwa akiugua ugonjwa mwingine,  alipofika pale aliandikiwa dawa za malaria, hali yake ikawa mbaya hadi akakimbizwa hospitalini kulazwa, tulipomuonya mmiliki hakutusikia,” alisema mmoja wa watu wanaoijua ishu hiyo kiundani.
Ili kupata ushahidi kamili, OFM ilijifanya mgonjwa na kwenda kwenye famasi hiyo kuomba ushauri wa matibabu.

Hausigeli huyo alimtajia dawa za typhoid lakini shushushu wetu alimkwepesha na kumuomba chloroquine ambapo hausigeli huyo alikubali na kutaka kumpa bila wasiwasi.

Baada ya kushuhudia hayo OFM ilimfuata mwenyekiti wa mtaa huo, Issa Shomari kupitia mjumbe wake na kufika katika famasi hiyo  kujionea hali halisi ambapo kama ilivyokuwa mwanzo hausigeli huyo alikuwa tayari kutoa huduma.
Baada ya kikosi kazi kujitambulisha na kumhoji, alikiri kuwa yeye ni mtumishi wa ndani,  ana miaka 16, elimu ya darasa la saba, mwenyeji wa Iringa, huwa anaachiwa auze na mwajiri wake huku akifunguka kuwa hutoa dawa za malaria na magonjwa anayoyafahamu.
Akizungumza kwa mshtuko baada ya kujionea hali halisi, mwenyekiti huyo wa mtaa alisema kuwa atahakikisha anawasiliana na kamati ya afya ya Wilaya ya Temeke, Dar ili kuziondoa famasi kama hizo mtaani kwake.

No comments:

Post a Comment