Blogger Widgets

July 18, 2013

Maajabu Mengine:Check Picha Jinsi Mtoto Mchanga alivyozaliwa na Tasbihi Shingoni Wakati akizaliwa Hosptali Kipindi Hiki cha Mwezi wa Ramadhani

Mtoto wa kike aliyezaliwa akiwa amevaa Tasbihi shingoni.

 

WAKATI leo kikiwa ni chungu  cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, kumeibuka maajabu,  mtoto wa kike amezaliwa akiwa amevaa Tasbihi shingoni.
Tukio hilo lilijiri katika hospitali binafsi ya uzazi kwenye Jiji la Kotaworo, eneo la Bida, jimboni Niger State  nchini Nigeria, Jumapili iliyopita ambapo maelfu ya watu walikusanyika kwa lengo kumshuhudia mtoto huyo.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Naija, mama wa mtoto huyo, Adijat alikimbizwa hospitali karibu na nyumbani kwa Alhaji Mohammed Bello Masaba, majira ya saa 8:00 mchana na baada ya pilika za uzazi, alifanikiwa kujifungua mtoto huyo.

Mmiliki wa hospitali hiyo ya uzazi, Alhaji Abubakar Baiwa Shasha ambaye ndiye aliyesimamia zoezi hilo la kujifungua alisema: “Nilishtuka nilipoona mtoto anatoka akiwa na Tasbihi nyeusi shingoni.

“Nilishangaa baada ya muda Tasbihi hiyo ilibadilika na kuwa nyeupe.”

Mara baada ya habari hiyo kusambaa, maelfu ya watu walifika hospitalini hapo wakisema: “Allahu Akibar…Allahu Akibar (Mungu mkubwa…Mungu mkubwa).

Baada ya taarifa hiyo ya ajabu kusambaa watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchini Nigeria walifurika kumwona mtoto huyo wengine wakimgusa.

Juhudi za kumpata baba wa mtoto huyo aitwaye Isah    zilishindikana.

No comments:

Post a Comment